Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta amesema serikali italifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATC) ili liweze kununua ndege nne na kuanza biashara.
Sitta
pia amesema Rais Jakaya Kikwete atazindua ujenzi wa reli ya kati kwa
kiwango cha `standard gauge’ itakayogharimu Sh16 trilioni huku akiwataka
viongozi wa vyama vya upinzani kuacha kuiba mipango ya serikali ya CCM.
Sitta
amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar ikiwa ni
siku chache baada ya mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa
wakati akifungua kampeni za chama hicho katika uwanja wa Jangwani,
alisema akichaguliwa atajenga upya reli ya kati na kufufua ATC.
Waziri
Sitta alisema anashangazwa na wapinzani kusema watajenga reli na
kufufua ATC wakati hiyo ni ni mipango ya serikali ya CCM ambayo
utekelezaji unaanza kabla ya uchaguzi.
Akifafanua,
alisema Rais Kikwete Septemba 15 mwaka huu atazindua ujenzi wa reli
katika eneo la Soga Mpiji wilayani Kisarawe na fedha hizo zitatoka
katika benki ya Rolthschild ya Marekani.
No comments:
Post a Comment