Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (wa kwanza
kushoto) akiwa kwenye hali ya furaha mara baada ya kuzindua msimu wa
saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15
mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja
na Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio
warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (mwenye shati jeupe), Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw.
Salim Kimaro (wa pili kulia) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano
NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Meneja
Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) warataibu wa mbio
hizo Bw Erasto Kilawe (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio
za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu
katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (wa pili
kushoto), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa tatu kushoto).
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw.
Salim Kimaro (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City
Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (wa kwanza kushoto) na Bi Ummy
Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa
mbio hizo.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (wa tatu kushoto)
akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji pamoja na wadhamini wa mbio za
Rock City Marathon mara baada ya kuzindua rasmi msimu wa saba wa mbio
hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika
Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine
ni (kutoka kushoto) Katibu Mkuu wa BMT, Lihaya Henry, Meneja Mkuu wa
kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio waratibu wa mbio
hizo, Erasto Kilawe, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro , Bi Ummy Hassan kutoka idara
ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo pamona na
Katibu Mkuu msaidizi chama cha riadha Tanzania (RT) Bi. Ombeni Savala .
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua msimu wa
saba wa mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika Novemba 15 mwaka huu
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbio
za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus
International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT),
pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na
kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani
kupitia sekta ya michezo.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Bw.
Malinzi alisema baraza linafuraha kuona makampuni binafsi yakijiingiza
katika kuinua mchezo wa riadha nchini.
“Mchezo
wa riadha una changamoto kubwa na tunatambua jitihada zinazoendelea
kufanywa na kampuni ya Capital Plus katika kurudisha hadhi ya mchezo
huu nchini kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini,” alisema.
Alisema
kuwa Tanzania itarudi kileleni katika medani za michezo duniani kama
wachezaji wataandaliwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
“Inashangaza
kuona taifa la watu milioni 45 linawakilishwa na wanariadha wachache
sana, tena katika mbio ndefu huku tukikosa wanariadha wanaoliwakilisha
vyema taifa katika mbio fupi,” alisema.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Meneja Mkuu kutoka kampuni ya Capital Plus
International, Bw. Erasto Kilawe alisema kuwa mbio hizo zimekuwa
zikionyesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.
“Jiji
la Mwanza limebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii. Jambo
hili limetusukuma kuendelea kumulika vivutio vya kipekee vinavyopatikana
katika ukanda wa ziwa Victoria kupitia mbio hizi,” alisema Bw. Kilawe
huku akiongeza kuwa mikakati kabambe imewekwa ili kuhakikisha mbio za
mwaka huu zinakuwa za mafanikio makubwa kuliko misimu iliyopita.
Alisema
baadhi ya makampuni yameanza kujitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni
pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Precision Air,
New Africa Hotel na Bank M huku makampuni zaidi yakionyesha nia ya
kudhamini mbio hizo.
“Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.
Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na
wanariadha, viongozi wa vyama vya riadha, viongozi wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) na wadau mbali mbali wa riadha nchini.
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF , Salim Kimaro alisema
kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kudhamini mbio hizo kutokana
ari yao katika kukuza hali ya michezo hapa nchini.
“Kwetu
suala la michezo ni moja ya vipaumbele vyetu kutokana na ukweli kuwa
michezo ni afya na pia ni sehemu ya ajira kwa vijana kwa sasa…tunaahidi
kuwa mstari wa mbele katika kufaanikisha mbio hizi,’’ alisema.