Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), na Afisa wa
Fedha Mwandamizi wa Mfuko huo, Angel Mukasa, (kulia), na Mfanyakazi mwingine wa
Mfuko huo, Omari Bundile, (wapili kushoto), wakigawa mafuta maalum yanayotumiwa
na watu wenye ulemavu wa ngozi, pamoja na sare za shule na viatu kwa wanafunzi
hawa wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini
jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2015. Katika kutekeleza sera ya mfuko ya
kusaidia jamii, PPF, imetoa vifaa mbalimbali ikiwemo, sare za snhule, viatu na
mafuta hayo maalum, Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Lulu Mengele aliwaambia
waandishi wa habari. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Latifa
Musa,(kulia), akitoa shukrani kjwa niaba ya wenzake baada ya watoto wenye
ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es
Salaam, kupatiwa msaada na Mfuko wa Pensheni wa PPF
Watoto
wenye ulemavu wa ngozi kwenye shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini
jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa msaada kutoka
Mfuko wa Pensheni wa PPF, shuleni hap oleo Ijumaa Septemba 11, 2015
Watoto
wenye ulemavu wa ngozi, wakiteta jambo, baada ya kupatiwa msaada wa vifaa
yakiwemo mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi
Picha ya pamoja ya maafisa wa PPF, Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu, Flora Millinga, akizungumza kwenye hafla hiyo
Lulu akiwa na baadhi ya watoto
Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akizungumza na watoto hao
wakati wa kutoa msaada wa vitu mbalimbali Septemba 11, 2015
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janet Ezekiel, (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya watoto hao
Kikundi cha Kwaya kikitoa burudani
Angel Mukasa, akizungumza na baadhi ya watoto
No comments:
Post a Comment