
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasilia katika mkutano wa hadhara wa kampeni,Korogwe vijijini.

MGOMBEA
urais kwa teketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo
kwa msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi
mkuu mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi
ya watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na
kutambua mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.
Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara
mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumishaamani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.
mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumishaamani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.

Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la
Bumbuli wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya leo.






Wakazi
wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa
Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni
ya leo.

Mgombea wa
Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kata
ya Magoma wakati akiwa njiani kuelekea Korogwe mjini kwenye mkutano wa
kampeni za CCM.

Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi
wa Mashewa wilayani Korogwe kwenye mkutano wa kampeni za CCM
ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kuchapa
kazi kwa maendeleo ya wananchi na nchi kwa jumla.

Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM
pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu
Stephen Ngonyani kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kwamazandu,
Korogwe Vijijini.

Bangozzzz

Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea
ubunge wa Jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya
CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya chuo cha ualimu
Korogwe.

Mwenyekiti
wa Wazazi CCM Taifa,Ndugu Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa
CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi katika uwanja wa
Togotwe-Mponde wilayani humo.

Wakazi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jioni ya leo,

Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi
wa Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea
barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha
Mponde.

Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi
wa Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea
barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha
Mponde.

Wananchi wakifuatilia mkutano.

Mgombea
Ubunge jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akifafanua jambo mbele ya
umati wa wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika viwanja vya Togotwe.

Wananchi wa Lushoto mjini wakishangilia jambo mara baada ya kumsikia Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia
No comments:
Post a Comment