NGUMI KUPIGWA CHANIKA SEPTEMBA 26 - LEKULE

Breaking

11 Sept 2015

NGUMI KUPIGWA CHANIKA SEPTEMBA 26

BONDIA Said Mbelwa anatarajia kupanda uringoni kwa mara nyingine tena kungombania mkanda wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa PST dhidi ya bondia George Dimoso mpambano utakaofanyika Septemba 26 katika ukumbi wa Butihama Villa Club uliopo chanika mpambano huo wa raundi kumi ulioratibiwa na
Kocha wa kimataifa nchini Rajabu Mhamila 'Super D' utakuwa ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wa kwanza Dimoso kudundwa kwa point
Super D aliongeza kuwa siku iyo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali itakayowakutanisha mabondia mbalimbali nchini ambapo
bondia Seleman Zugo atapambana na Abdallah Ruwanje na Adam Ngange atakabiliana na Shabani Mtengela na Said Uwezo atapambana na Hassan Mgosi uku Hamza Mchanjo ataoneshana kazi na Ally Maiyo mipambano yote ya utangulizi ni ya raindi sita
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha.

No comments: