Mvua ya mawe yasababisha madhara makubwa mjini ngara mkoani Kagera. - LEKULE

Breaking

3 Sept 2015

Mvua ya mawe yasababisha madhara makubwa mjini ngara mkoani Kagera.

Siku moja baada ya mamlaka ya hali ya hewa nchini kutoa tahadhali ya mvua kubwa katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera imenyesha mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha maafa makubwa ambapo kaya 312 zimeathirika vibaya kwa kukosa chakula baada ya mashamba yao kusombwa na maji huku familia sita zikikosa makazi na baadhi ya majengo ya shule ya msingi na jengo moja la halmashauri ya wilaya kuezuliwa na upepo.
Mvua hivyo iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili jioni imesababisha madhara makubwa kwa wananchi wa mji wa Ngara ambapo mashamba ya migomba ya ndizi yamehalibiwa vibaya huku nyumba zikiezuliwa na upepo ambapo  ITV imezungumza na afisa mtendaji wa kata ya Ngara mjini Bw.Yothamu John amesema kuwa mvua hivyo imesababisha madhara makubwa kwa jamii.
 
Baadhi ya waathirika wa mvua hivyo wameiomba serikali kuwasaidia misaada mbalimbali ikiwemo chakula ili kunusuru maisha ya watu wanaokabiliwa na janga la njaa kutokana na mazao waliyokuwa wakitegemea kwa chakula kusombwa na maji.

No comments: