Mkurugenzi
wa Maendeleo wa Don Bosco Tanzania ,Celestine Kharkongor (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Don Bosco Oyterbay
jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo na shughuli zinazofanywa
na Don Bosco hapa nchini.
Meneja
Mipango wa Ofisi ya Maendeleo Don Bosco Tanzania, Rosemarytery Njoki
(kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi
wa Maendeleo wa Don Bosco Tanzania ,Celestine Kharkongor, Mratibu wa Don
Bosco, Maika Denys na Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans.
Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Don Bosco, Maika Denys (kulia), akichangia jambo.
Mwalimu wa Don Bosco, Hellen Jackson (kulia), akielezea mafanikio makubwa wanayopata wanafunzi katika shule hiyo.
Ofisa Mwezeshaji Aira wa Don Bosco Tanzania, Oswald Manyerere (kushoto), akielezea jinsi Don Bosco ilivyofanikiwa kuwatafutia ajira wanafunzi wao waliohitimu mafunzo mbalimbali.
Mkuu wa Idara ya Utafuta wa ajira na Ofisa Masoko, Don Bosco Dar es Salaam, Nyerembe Yunus Nyampiga (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mmoja wa wanafunzi wa DonBosco akielezea mafanikio wanayopata shuleni hapo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanafunzi na walimu wao wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanafunzi wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Viongozi wa Don Bosco wakiwa meza kuu.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari na Wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
MKUTANO
wa Nne wa Bara la Afrika wa kujadili mipango endelevu katika eno la
mafunzo kwa vijana na wataalamu wasiojiweza na ushirikji wao katika
soko la ajira, unatarajiwa kuanza kufanyika kesho Hoteli ya Girrafe
jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao utashirikisha nchi mbalimbali tisa unatarajiwa kuhudhuriwa na wageni 50 kutoka katika nchi hizo za Afrika.
Akizungumza
na waaandishi wa habari kuhusu Dar es Salaam jana kuhusu mkutano huo,
Meneja Mipango wa Ofisi ya Maendeleo Don Bosco Tanzania, Rosemarytery
Njoki alisema, mkutano huo utatoa nafasi kwa Mtandao wa Don Bosco
Afrika kuchunguza njia ambazo zitaleta ushirikiano mzuri kati ya sekta
binafsi na umma ili kuleta maendeleo zaidi.
“Mkutano
unatarajiwa kutafakari juu ya mipango inayoendelea katika eneo la
mafunzo ya kijamii na wataalamu vijana wasiojiweza na ushiriki wao
katika soko la ajira. Kama vile namna bora ya washirika wanaweza kufanya
kazi na binafsi na ya umma sekta kuelekea maendeleo endelevu,” alisema
Njoki.
Alisema
mkutano huo pia utazungumzia masuala ya jinsia hasa kwa upande wa
upatikanaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kuwafanya wanawake kuwa sawa
na wanaume kwa kufanya kazi sawa.
“Pia
tunatafuta kubadilishana uzoefu na washirika weu wa Afrika ambao wote
tunafanya kazi ili kuboresha elimu, masuala ya mafunzio ya ufundi stadi
na kuwaunganisha vijana na masoko ya ajira ya dunia,” alisema.
Alisema
kwa mara ya kwanza mkutano huo unafanyika nchini kuanzia leo hadi
Septemba 25, utakuwa ni kwa ajili ya ushirikiano wa sekta binafsi na
umma. Alisema mkutano huo pia utawakutanisha shirikisha watu mbalimbali
ikiwemo taasisi za serikali na chuo cha VETA.
Kwa
upande wake Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans alisema, mkutano
huo pia utatumika kuangalia njia ambazo Don Bosco inaweza kutumia
kushirikiana zaidi na sekta binafsi kama sehemu ya mipango endelevu.
Alisema majadiliano mengine yatakuwa yanahusu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi namna ya kushirikiana ili kuboresha elimu.
Ofisa
Mwezeshaji Aira wa Don Bosco Tanzania, Oswald Manyerere alisema, lengo
la mafunzo yanayotolewa na tasisi hiyo ni kuhakikisha wanawawezesha
vijana wasiojiweza kupiga hatua na hatimaye kufikia malengo
waliyojiwekea.
Alisema
vijana wanaopitia katika chuo hicho wamekuwa wakitafutiwa kazi baada ya
kufanya mafunzo yao, ambapo kwa kipindi cha mwaka jana vijana
waliomaliza walikuwa ni 322 na hadi sasa waliopatiwa kazi ni 220 huku
idadi kubwa ikiwa ya wasichana sawa na asilimia 86.
Alisema wanafunzi hao ni kutoka katika shule zilizochini ya Don Bosco, Dodoma, Iringa na Oyterbay Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco,Celestine Kharkongor alisema Don Boscow ilianza hapa nchini mwaka 1996.
Alisema tangu kuanzishwa kwa chuo cha Don Bosco kimeleta mabadiliko ya tabia kwa vijana pamoja na kuwakwamua kiuchumi.
Mwalimu
wa Don Bosco, Hellen Jackson alisema mafunzo yanayotolewa na chuo cha
Don Bosco yatasaidia kutoa ajira kwa vijana na kuondoa changamoto
zilizopo sasa za ukosefu wa ajira hapa nchini.
Alisema wazazi wenye watoto wa kike ni fursa kwao kuwapeleka katika chuo hicho