Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi kutoka Kinyelezi I kwenda katika mitambo ya Ubungo I na II, jijini Dar es Salaam imekamilika.
Aidha,
kazi ya kuwasha mashine 10 za mtambo wa Ubungo I imekamilika na
inategemewa tatizo la kukatika umeme litafikia tamati kuanzia leo.
Akizungumza
na mtandao huu jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Tanesco,
Adrian Severin, alisema kazi ya kuwasha mitambo hiyo inahitaji umakini
mkubwa kutokana na mfumo unaotumika kuwa mpya.
Alisema
kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi imekamilika na tatizo lililokuwapo
la kukatika umeme lilitokana na matengenezo ya mfumo mpya yaliyokuwa
yakiendelea kwa ajili ya kuwashwa kwa mitambo hiyo mipya.
Aliwataka
wananchi wawe na subira wakati kazi hiyo ikiendelea na hadi kufikia leo
itakuwa imekamilika na umeme utapatikana kwa uhakika baada ya kuanza
kuzalishwa kwa kutumia gesi kutoka Mtwara.
“Kuanzia
leo (jana) umeme umeanza kurudi kupatikana kwa uhakika katika mikoa
mbalimbali pamoja na jiji la Dar es Salaam kutokana na mafundi
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasha genereta 10 za Ubungo I, hivyo
mpaka kesho (leo) uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka,” alisema na kuongeza:
“Watanzania
wategemee umeme wa uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme wa gesi ya
Mtwara kwani kazi ya kuunganisha bomba la kusafirisha nishati hiyo
imekamilika hivyo inatuhakikishia nchi kuwa na umeme wa uhakika hata
kama mabwawa ya maji yanayotumiwa kuzalisha umeme yatakuwa yamekauka.”
Severin
alisema gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II
wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi
I, MW 150).
Alisema
mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya
Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa
inatosha kuendesha mitambo hiyo.
Severine
alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa
takribani dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka, ambazo zilikuwa
zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha
No comments:
Post a Comment