Magufuli awasha moto Shinyanga - LEKULE

Breaking

27 Sept 2015

Magufuli awasha moto Shinyanga


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati umefika wa kujenga Tanzania mpya yenye viwanda vya kutosha kutoa ajira kwa vijana wengi.
Alisema pia kuwa Serikali yake itakuwa rafiki wa sekta binafsi na kuwajengea uwezo wafanya biashara ndogo ndogo ili waweze kujiendeleza.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wake wa Kampeni ambapo aliwaambai wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi kwa maendeleo ya nchi.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele kwenye mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Kambarage.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao Mgombea urais anazo changamoto za Shinyanga mjini na anaamini atazitatua hivyo amewataka watu wake kumpa kura nyingi za Dk. John Pombe Magufuli ifikapo tarehe 25 Octoba
 Wasanii wakipiga push up jukwaani kabla ya mgombea wa urais kupitia CCM hajahutubia.


 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Mzee Samuel Sitta akihutubia wakazi wa mkoa wa Shinyanga kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa mji wa Shinyanga mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Kambarage.
 Wananchi wa Jimbo la Solwa wakimsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli