Maelfu ya
wahamiaji waondoka kwa mguu kutoka kituo kikuu cha treni cha Budapest
wakielekea kwenye mpaka wa Austria, Septemba 4, 2015
Maelfu ya
wahamiaji wameondoka mapema leo Ijumaa alasiri kutoka kituo kikuu cha
treni cha Budapest wakijaribu kutembea kwa mguu wakielekea "Austria",
baada ya viongozi wa Hungary kuchukua uamzi Jumanne wiki hii wa
kusimamisha usafiri wa kimataifa kwa kutumia reli, ameshuhudia mwandishi
wa AFP.
Wahamiaji,
ambao baadhi yao walikuwa wamekwama katika mji mkuu wa Hungary kwa siku
kadhaa, wamesema wanataka kutembea kwa mguu hadi kwenye mpaka wa
Austria, ulio kwenye umbali wa kilomita 175, wakati serikali ya Budapest
imeongeza jitihada za kuwahamisha kinyume na matakwa yao katika makambi
ya mapokezi ya kwanza.
Wahamiaji,
ikiwa ni pamoja na watoto na watu wanaotumia viti vya magurudumu,
wamevuka moja ya daraja kuu katika mji wa Danube bila hofu ya kukamatwa
na vikosi vya usalama.
Hungary,
moja ya nchi kuu wanakopitia wahamiaji kwa kwenda Ulaya ya Kati,
kuulionekana wahamiaji wapya 3,300 wakiwasili kwa siku moja pekee ya
Alhamisi, shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi
limebaini leo Ijumaa.
Wakati
huo huo Aylan, mtoto mdogo kutoka syria aliyefariki baada ya kuzama
katika bahari wakati alipokua akijaribu kukimbia kufuatia mapigano
nchini Syria, amezikwa le Ijumaa na familia yake, lakini tukio hilo la
kusikitisha ambalo ni ishara kwa mgogoro wa wahamiaji limeendelea kuzua
migawanyiko kati ya nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment