(Kigamboni-Dar
es Salaam) Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) ambaye pia anapeperusha bendera ya UKAWA inayoungwa mkono na
vyama vya NCCR-Mageuzi, NLD, CHADEMA na CUF, Kamanda Lucy Magereli
amewataka wananchi wa jimbo hilo la Kigamboni kumpigia kura za ndio
hiyo Oktoba 25, mwaka huu ili aweze kwenda kutetea kero zao mbalimbali.
Lucy
Magereli anaeleza kuwa, wananchi wa jimbo hilo wanataka mabadiliko hasa
kwa kupelekewa maendeleo na si porojo kama wafanyavyo Chama tawala
ambacho kimeshindwa kuwatetea kwa zaidi ya miaka mingi huku kikiendelea
kuwanyonya na hata kupokonya haki zao ikiwemo Ardhi. Pia imeshindwa
kutekeleza huduma bora za kielimu, Afya na miundombinu zaidi ya miaka
mingi huku hata wakipeleka huduam hizo ni chini ya kiwango.
“Kila
mwana Kigamboni. wakati wa mabadiliko ni huu. Oktoba 25, mapema naomba
kura yako..Tuichague CHADEMA kwani ndio mkombozi wa kweli na Mabadiliko
tunayoyataka ni sasa” alieleza Lucy Magereli.
Lucy
Magereli anaendelea kuchanja mbuga katika maeneo mbalimbali ya Jimbo
hilo la Kigamboni huku akiwatak wananchi kujitokeza kwa wingi kusikiliza
sera na kumuunga mkono.
Chadema mwendo mdundo Jimbo la Kigamboni…


No comments:
Post a Comment