ZIKIWA zimebakia siku 30 kabla watanzania hawajapiga kura ya kumchagua Rais,mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa ambaye amekuwa akieleza imani yake kuwa atashinda kwa kishindo, ameeleza msimamo wake endapo tume ya Taifa ya Uchaguzi itatangaza matokeo tofauti na ya matarajio yake.
Akiongea
na kituo cha Runinga cha Citizen cha nchini Kenya, Lowassa
amesema hawezi kusema kama atakubali au atakataa hadi
itakapothibitika kuwa matokeo hayo hayajahujumiwa.
"Siwezi
sema nitakuchukulia kama nimeshindwa hadi nitakapothibitishiwa
kuwa kila kitu kimeenda sawa na kwamba hakuna hujuma." Alisema Lowassa na kuongeza;
"Tunaogopa
sana kuhusu hujuma.Kila mtu unayeongea naye unapokutana naye,
anakwambia utashinda, lakini je, watakubali kushindwa?"
Katika
hatua nyingine,Lowassa alijibu swali la mwandishi lililomtaka
kueleza kama angeweza kusema anachokisema hivi sasa kuhusu CCM
endapo angechaguliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
"Ninasema
vitu vingi ambavyo vingeweza kufanywa vizuri zaidi na CCM,na
ninasema vitu vingi ambavyo ninaweza kuvifanya vizuri zaidi
nikiwa Upinzani." alisema Lowassa.
Tazama Video Hapo Chini kumsikiliza