Ni siku chache tu zimepita, Tanzania imesheherekea siku ya utalii duniani kwa kauli mbiu “Mamilioni ya watalii ni mamilioni ya fursa” ambapo kauli mbiu hii imekuwa na lengo zuri la kuweka vipaumbele vya kimaendeleo katika sekta ya utalii Tanzania.
Tanzania,
kati ya nchi za Umoja wa Mataifa, huadhimisha siku kuu hii kila tarehe
27 ya mwezi Septemba ya kila mwaka, kwa lengo kubwa la kuhamasisha
uelewa juu ya sekta ya utalii na mchango wake katika jamii.
Ban Ki-moon, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alifafanua kwamba, “utalii
unaleta fursa nyingi kwa kuajiri watu wengi na kukuza uchumi wa nchi
kupitia mabilioni ya watalii wa kimataifa wanaosafiri kila mwaka”. (Redio ya Umoja wa Mataifa)
Hata hivyo, Tanzania
imekuwa ikishehereka siku kuu hii kila mwaka, lakini bado kumekuwa na
ufahamu mdogo kuhusiana na sekta hii ya utalii hasa kwa watanzania wasio
na desturi ya kutembelea maeneo ya hifadhi ya taifa.
“Kwa
kuwa asilimia 33 ya eneo la nchi ni maeneo yaliyohifadhiwa kisheria
ikiwemo misitu na wanyamapori, Tanzania inabidi iwe mstari wa mbele
katika ufuatiliaji wa kauli mbiu hiyo ikiwemo kuboresha sehemu muhimu
kama hoteli za kitalii na hifadhi za taifa kwa kuangalia kama zinakidhi
viwango vya kushindanishwa na nchi za jirani”. Andrea Guzzoni,Meneja mkazi wa JovagoTanzania aliafafanua.
Hata
hivyo bado tunahitaji kuangangalia changamoto nyingine nyingi
zinazoikabili sekta hii, ikiwemo ujangili na biashara haramu ya nyara,
migogoro ya mipaka na uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya taifa, pamoja na
uhaba wa elimu ya kutosha juu ya utunzaji wa misitu na hifadhi za taifa,
alifafanua.
Kwa upande wake Lilian Kisasa, Afisa meneja mawasiliano wa JovagoTanzania aliongeza kwa kusema kuwa, “mwisho
wa kauli mbiu hii sio siku ya utalii duniani peke yake, inabidi kutilia
mkazo hasa katika utendaji wa kazi kuanzia ngazi ya familia, kijana au
jami kwa ujumla itambue kuwa sekta hii ni utambulisho tosha wa madhari
na sura ya taifa yetu. Serikali na sekta binafsi ni jukumu letu
kuhakikiksha miundo mbinu kama barabara, viwanja vya ndege, na madaraja
kwa mwaka 2016 ziwe katika sura mpya”.