Kutoka kushoto ni viongozi wa CEMOT, Meneja mradi, Bernard Kindoli na Balozi wa Den mack, Etnar Jensen.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti mwenza kutoka Tanzania Civil Society Consortium on
Election Observation (TACCEO), Martina Kabisama, Meneja mradi, Bernard
Kindoli na Balozi wa Den mack, Etnar Jensen.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Balozi wa Den mack, Etnar Jensen akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari. (P.T)
Asasi za
kiraia zinazofuatilia na kuangalia chaguzi nchini Tanzania zimeunda
muungano unaoitwa Coalition on Election Monitoring and Observation in
Tanzania kwa kifupi CEMOT. CEMOT inaendeshwa kwa ushirikiano baina ya
TEMCO (Tanzania Election Monitoring Committee) na TACCEO (Tanzania Civil
Society Consortium for Election Observation). Lengo kuu la CEMOT ni
kuongeza ushiriki wa wananchi katika kufuatilia na kuangalia mchakato wa
uchaguzi ili kuwa na fursa ya kuhakikisha uhalali (credibility) wake.
Kwa kuwa
CEMOT inakusudia kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)
katika kupata taarifa mbali mbali za matukio yanayohusu uchaguzi kutoka
kwa waangalizi wa ndani na wananchi kwa ujumla, imetengeneza Kituo cha
Ufuatiliaji wa Uchaguzi (Tanzania Election Observation Centre).
Lengo kuu
la kituo hiki ni kuongeza ushiriki wa wananchi katika kufuatilia na
kuangalia Uchaguzi Mkuu wa 2015. Pia ni kuwapa wananchi fursa ya
kuwasiliana moja kwa moja na taasisi za Serikali zinazohusika na
usimamizi wa uchaguzi. Taasisi hizo ni kama vile Tume ya Uchaguzi ya
Taifa, Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Polisi
Zanzibar, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa, Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar, Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Seriali, na
nyinginezo.
CEMOT
inaamini kuwa kwa kufikisha taarifa kwa wakati kwa wadau na mamlaka za
uchaguzi kutadumisha utulivu na maelewano kabla, wakati na baada ya
uchaguzi.Ufunguzi wa kituo cha CEMOT cha Ufuatiliaji wa Uchaguzi
unaofanyika kuanzia leo Septemba 2, 2015 kuanzia saa tisa mchana katika
ukumbi wa Hoteli ya Southern Sun Dar es Salaam.
Uzinduzi
huo utahudhuriwa na wadau wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi,
wachambuzi nguli wa masuala ya uchaguzi, waangalizi wa ndani na nje
pamoja na wanachi waalikwa. Pia kutakuwa na mabalozi wa nchi mbalimbali
pamoja na wawakilishi wa taasisi zinazoshugulika na uangalizi wa
uchaguzi.
CEMOT
inaamini kituo hiki kitasaidia kusaidia kuboresha mchakato wa uchaguzi
wa mwaka 2015 na chaguzi nyingine zitakazofuata kwa kutoa fursa kwa
wananchi kuwasiliana moja kwa moja na vyombo husika kunapokuwa na
tatizo.
Kituo
hiki kinatarajia kufanya kazi kwa kushirikiana na waangalizi wa uchaguzi
wa muda mfupi wapatao 10,000 katika vituo mbalimbali, waangalizi wa
uchaguzi wa muda mrefu wapatao 350, timu za wataalamu wa TEHAMA pamoja
na wachambuzi wa uchaguzi kwenye uwanda wa siasa, sharia, habari, na
jinsia.
Kituo hiki cha kidigitali kitapatikana katika wavuti ya www.uchaguziwetu2015.org pamoja na
Twitter: uchaguziwetu15
Facebook: uchaguziwetu2015
Instagram: uchaguziwetu2015
Youtube: uchaguziwetu2015
Email: sema@uchaguziwetu2015.org
Kauli
mbiu yetu ni: andaa, shirikisha na jishirikishe kwa uchaguzi wenye
uhalali, huru na haki (generate, share, engage. credible, free and fair
elections)
Shughuli
ya Uzinduzi wa Kituo cha Ufuatiliaji wa Uchaguzi, utatanguliwa na
ufunguzi wa ofisi za CEMOT zilizopo katika Jengo la GEPF barabara ya Ali
Hassan Mwinyi (mkabala na kituo cha mafuta cha Victoria), Ghorofa ya
Saba.
Imetolewa na
CEMOT
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
02.09.2015
No comments:
Post a Comment