Raisi
Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa nchi za Afrika kuipa nguvu
mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu iliyoko jijini Arusha ili iweze
kusikiliza za kesi za jinai badala ya kupelekwa moja kwa moja kwenye
mahakama ya kimatifa ya makosa ya jinai.
Kikwete
amesema kuwa iwapo Mahakama hiyo itapewa nguvu itarahisisha
upatikanaji wa haki za raia katika bara la Afrika na kuimarisha misingi
ya utawala bora na kuheshimu haki za Binadamu.
Akihutubia
Mahakama hiyo jana Raisi Kikwete alizindua kitabu chenye taarifa
muhimu za mahakama hiyo kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ,amesema
kuwa ni hatua mojawapo katika kuhakikisha lugha hiyo inatumika
mahakamani hapo na kuwawezesha Watanzania wengi na Waafrika kuelewa
shughuli za mahakama hiyo na utendaji kazi wake.
Raisi
wa Mahakama hiyo Jaji Agustino Ramadhani amesema kuwa itachukua muda
mrefu kwa mahakama hiyo kuanza kusikiliza kesi za jinai kwani bado
nchi nyingi za Kiafrika hazijaidhinisha mkataba wa Malabo uliotolewa
tangu Juni mwaka jana ili kuanzisha hatua za usikilizwaji wa kesi za
jinai.
“Mpaka
sasa hakuna nchi hata moja iliyoidhinisha mkataba wa Malabo ambao
ulitolewa tangu juni mwaka jana hivyo itachukua muda mrefu mpaka
mahakama iweze kusikiliza kesi za jinai” Alisema Jaji Ramadhani
Ziara
ya Raisi Kikwete kutembelea Mahakama hiyo imetajwa kuwa ziara ya Mwisho
ya Raisi huyo katika kipindi cha Uongozi wake unaolekea tamati lakini
pia ni ziara ya kwanza ya Rais huyo tangu kuanzishwa kwa Mahakama ya
Afrika.
No comments:
Post a Comment