Mwenyekiti
wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya
Kiafya, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa Ijumaa wiki hii
kuwasilisha mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa
maendeleo ya kazi ya Jopo tangu lilipoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Ban Ki Moon, mwezi April mwaka huu.
Na MwandishiMaalum, New York
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya Juu
kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya, anatarajiwa Ijumaa
wiki hii, kuelezea mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa
Mataifa kuhusu maendeleo ya kazi ya jopo hilo tangu kuundwa kwake.
Jopo
la Ngazi ya juu kuhusu mwitiko wa Kimataifa wa majanga ya kiafya
liliundwa mwezi wa nne mwaka huu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki
Moon, ambapo Rais Kikwete amepewa jukumu la kuongoza jopo hilo.
Taarifa
ambazo zimeufikia Uwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa, zimebainisha kuwa Mhe.
Rais atawazungumza na wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mara
baada ya kumalizika kwa mkutano wa tatu wa jopo hilo unaofanyika hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wengine wa Jopo hili ni Bw.
Celso Amorim( Brazil), Micheline Calmy ( Switzerland), Marty Natalegawa ( Indonesia) Joy Phumapi ( Botswana) na Rajav
Shah ( USA).
Jukumu
kubwa ya jopo hilo kwa mujibu wa hadidu rejea,pamoja na
mambo mengine,ni kutoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha mifumo ya
kitaifa na kimataifa katika kuzuia na kukabiliana na majanga ya kiafya
ikiwa ni pamoja na kujifunza kuhusu mwitikio wa Jumuiya ya Kimataifa
kufuatia kuibuka kwa janga
la ugonjwa wa Ebola.
Katika utekelezaji wa majukumu yake Jopo limekuwa likikutana na kufanya majadiliano ya
kina na makundi mbalimbali ya kiwamo ya wataalamu, wawakilishi wa nchi tatu ambazo zimeathirika sana na ugonjwa wa ebola
( Liberia, Siera Leonena Guinea),Mashirika ya Kimataifa na Kikanda
, Taasisi za Fedha za kimataifa, wahudumu wa Afya, Wasomi ,Watafiti, Sekta Binafsi na wataalam wa fani na kada mbalimbali.
Pamoja
na kuhudhuria na kuongoza mikutano ya Jopo,
Mhe, Rais Kikwete akiwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
pia atahudhuria Mikutano Mikubwa miwili ambayo ni, Mkutano wa Kilele wa
Kisiasa, ambao Wakuu wa Nchi na Serikali watapitisha Malengo ya
Maendeleo Endelevu
( SDGs). Mhe.
Rais atazungumza katika mkutano huu muhimu kwa mstakabali wa maendeleo
na ustawi wa binadamu kwa miaka
15 ijayo.
Malengo Mapya ya Maendeleo ya nachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia(
MDGs) yanayomaliza muda wake mwishoni mwa mwaka.
Aidha Mhe. Rais atashiriki na kuhudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Na anarajiwa kuzungumza na Baraza Kuu na hii itakuwa ni hotuba yake ya mwisho akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Vile
vileMhe.
Rais atahudhuria mikutano mingine kadhaa. Baadhi ya mikutano hiyo ni ule
ambao umeandaliwa kwa pamoja baina ya Kansela wa Ujerumani Mhe.
Angela Merkel , Waziri Mkuu wa Norway
Mhe. Erna Solberg na Rais wa Ghana Mhe.
John Dramani Mahama.
Mhe Rais anahudhuria mkutano huu kwa mwaliko rasmin aliopewa na Kansela
Angela Markel.
Mkutano
huu unatarajiwa kuzindua misingi na hatua muhimu ambazo zinataratibu
ufanisi na upimaji wa matokeo ya juhudi za kuimarisha mifumo ya afya.
No comments:
Post a Comment