Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Chuo cha
Ukamanda na unadhimu Dukuti nje kidogo ya mji wa Arusha Septemba 13,
2015
Mkuu wa
Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Meja Jenerali Ezekiel Kyunga kulia
akimuonyesha Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeneo
mbalimbali ya Chuo hicho muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua Chuo
hicho eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo.Kushoto ni Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vitabu katika maktaba
ya Chuo cha Unadhimu na Ukamanda alichokizindua Septemba 13, 2015.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mitaala
inayofundishwa katika chuo cha Ukamanda na Unadhimu katika moja ya
kompyuta chuoni hapo muda mfupi baada ya kuzindua chuo hicho eneo la
Duluthi nje kidogo ya mji wa Arsuha leo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho
Meja Jenerali Ezekiel Kyunga.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa ushauri wakati akikagua majengo ya Chuo
Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa
Arusha leo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda,kushoto ni Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Wapili kushoto ni Mkuu wa chuo
hicho Meja Jenerali Ezekiel Kyunga na kulia ni mwakilishi kutoka Umoja
wa Falme za Kiarabu Balozi Ibrahim Al Suweidy.umoja wa Falme za Kiarabu
ulishirikiana na Serikali kufadhili ujenzi wa Chuo hicho.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Unadhimu na ukamanda.
No comments:
Post a Comment