23 Sept 2015

Jaji Warioba amnadi mgombea wa jimbo la Kawe Kippi Warioba

 Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akimnadi Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumapili Sept. 20.15. Kushoto ni Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Charles William Iteba.  PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akizungumza wakati akiwanadi Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia) na Mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo, Charles William Iteba  katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akipongezwa na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia  mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akiagana na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia  mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Kippi Warioba akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Kippi Warioba akibadilishana mawazo na Mmoja wa makada wa CCM waliohudhuria mkutano huo. Kulia ni Mkewe Nkaleni Warioba.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Zarina Madabida akiongozana na Kippi baada ya mkutano kumalizika.
Mtoto akiwa bango lenye picha ya Kippi Warioba.

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, amesema anafahamu changamoto zinazowakabili wamachinga, mamalishe, baba lishe na wajaririamali wadogo; na kuomba wamchague ili azishughulikie.
Aidha, baba mzazi wa mgombea huyo, Jaji Joseph Warioba, amewataka wakazi wa Kawe wamchague kijana wake kwa kuwa ni msikivu, anayejituma na siyo mtu wa kusukumwa.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Songas ulipo Kata ya Makongo Juu juzi, Kippi alisema amewahi kufanyakazi na sekta binafsi ambayo ilimkutanisha na wajasiriamali, vikundi vya ujenzi, Saccos na Vicoba, hivyo alifanikiwa kujua changamoto zinazowakabili.
“Changamoto za makundi haya nazifahamu, nafahamu mnahitaji mafunzo na rasilimali mbalimbali kuendesha biashara zenu nithibitisheni Oktoba 25 nikazifanyie kazi,” alisema.
Kuhusu Makongo Juu, Kippi alisema Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, imeainisha kwamba barabara ya Makongo kuanzia Chuo cha Ardhi hadi Goba itajengwa kwa kiwango cha lami na tatizo la maji litakwisha kwa kuwa serikali itakamilisha mradi wa kutoa maji Kimbiji hadi Dar es Salaam.
“Matatizo ya michango mingi shuleni ambayo wazazi wanailalamikia, uhaba wa madawati, matundu ya vyoo, vitabu na madawati ni mambo ambayo tutashirikiana kwa pamoja kuyatatua wala hayahitaji mipango mikubwa ya serikali,” alisema.
Alisema wakazi wa Kawe wanapaswa kumchagua Dk. John Magufuli, yeye (Kippi) pamoja na madiwani wa CCM ili wakamsaidie kazi ya kutekeleza ilani.
Naye Jaji Warioba alisema wakazi wa Kawe hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani kwa kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Magufuli, itafanyakazi nzuri.
Alisema Dk. Magufuli ni mtendaji mzuri asiyependa rushwa hivyo ni wajibu wa wananchi kumchagulia wasaidizi kutoka CCM ili wakafanyekazi ya kuwatumikia.

Alisema hulka za Dk. Magufuli zinafanana na za mtoto wake (Kippi), kwa kuwa naye ni mchapakazi, msikivu na mtu mwenye ushirikiano mkubwa.

Naye mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo Juu, William Iteba, alisema kero za wakazi wa kata hiyo zinajulikana ikiwamo ukosefu wa kituo cha polisi, soko na ajira; hivyo akichaguliwa atatatua kero hizo.