Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana jana baada ya kushikiliwa na polisi juzi.
Polisi mkoani Arusha walimkamata mwanasiasa huyo pamoja na watu wengine wanne juzi jioni mara baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo kwa awamu ya pili katika Shule ya Msingi Ngarenaro.
Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao.
Mwanasiasa huyo na wenzake wameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana waliyowekewa.
No comments:
Post a Comment