Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wananchi
katika moja ya mikutano ya kampeni Wilaya ya Newala mkoani Mtwara.
|
Aliyekuwa mbunge wa
Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wananchi na wanaCCM katika mkutano
wa kampeni wa mgombea mwenza, Bi. Samia Hassan Suluhu Mtwara Vijijini. |
|
Baadhi ya wanaCCM na
wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa
kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan Suluhu. |
|
Mgombea mwenza wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika moja
ya mikutano ya kampeni Mtwara Vijijini. |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekubali ombi la msemaji wa kambi ya
ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA la kufanya mdahalo wa wazi kati
ya wagombea urais wa nafasi za urais yaani John Pombe Magufuli wa CCM na
Edward Ngoyai Lowassa wa CHADEMA.
Kauli ya CCM imetolewa leo na mgombea mwenza wa urais Chama Cha
Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu katika hotuba zake alizozitoa kwa nyakati
tofauti kwenye mikutano yake ya hadhara ya kampeni ya CCM aliyoifanya
Wilayani Newala na Jimbo la Mtwara Vijijini.
Bi. Suluhu alitoa kauli hiyo akijibu hoja ya kambi ya UKAWA
iliyotolewa jana na msemaji wa kambi hiyo, James Mbatia alipokuwa
akizungumza na vyombo vya habari jana akieleza kuwa kuna haja ya kuomba
mdahalo wa wazi kati ya wagombea hao kwa lengo la kuwasikia nini
wanataka kuzungumza.
Mgombea huyo mwenza alisema Chama Cha Mapinduzi kipo tayari kufanya
mdahalo na mgombea wa CHADEMA, lakini ikiwa mdahalo huo utakuwa kati ya
wagombea hao ili kuwapa nafasi ya kujieleza kiunaga ubaga kujua nini
wagombea hao watajitolea kufanya ili kuendelea jamii ya Watanzania
endapo wakifanikiwa kuingia madarakani.
Mgombea huyo mwenza akifafanua zaidi katika mikutano yake ya kampeni
Jimbo la la Mtwara Vijijini alisema Serikali ya CCM imepanga kuijenga na
kuiboresha Bandari ya Mtwara ili iweze kuleta tija zaidi kwa watumiaji
wake. Aliongeza kuwa Serikali ya CCM endapo itapita imepanga kujenga
barabara ikiwemo ya Mtwara-Newala- Masasi, hospitali, pamoja na
kuukamilisha mradi wa ‘Makonde Water Sapply’ ambao unasaidia kuleta maji
mjini.
Alisema kwa wakulima wa korosho Serikali itakuwa ikitoa pembejeo na
dhamana kwa mahitaji ya wakulima ili kuchochea uzalishaji wa wakulima.
Alisema dhana ya ruzuku za kilimo itatekelezwa kwa upangilio maalumu kwa
lengo la kumuwezesha mdhamini.
Mgombea mwenza huyo amekuwa akipata wakati mgumu njiani akitokea
Mtwara mjini kuelekea Wilaya ya Newala ambapo wananchi wamekuwa
wakifunga barabara kumsimamisha ili aweze kuzungumza nao, huku wakitaja
baadhi ya kero katika maeneo yao wakiomba azitatuwe endapo atafanikiwa
kuunda dola.
|
Mgombea mwenza Bi.
Samia Suluhu akimtambulisha na kumuombea kura mgombea Ubunge, Mathias
Chikawe katika moja ya mikutano ya kampeni. |
|
Mgombea mwenza wa CCM
nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge
wa chama hicho Rashid Akbar (kulia). |
|
Baadhi ya wagombea udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitambulishwa kwenye mkutano wa kampeni. |
|
Mgombea
mwenza Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na wanachama na wananchi
mara baada ya kuzinduwa tawi la wakereketwa la Kitama 1. |
|
Mgombea mwenza Bi.
Samia Suluhu (katikati) akizungumza na wanachama na wananchi mara baada
ya kuzinduwa tawi la wakereketwa la Kitama 1. |
|
Bi. Samia Suluhu
katikati akipokea kadi ya mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi baada
ya uzinduzi wa Shina la Wakereketwa Kitama 1, Mtwara Vijijini. |
|
Baadhi
ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan
Suluhu. |
|
Baadhi
ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan
Suluhu. |
|
Mmoja mwa makada wa CHADEMA, Greison Mtemi Nyakarugu ambaye kwa sasa yupo Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM. |
|
Baadhi
ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan
Suluhu. |
|
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika moja ya mikutano ya kampeni Mtwara. |
|
Mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM na wananchi
katika moja ya mikutano ya kampeni Wilaya ya Newala. |
|
Baadhi ya vijana wanaCCM wakizunguka wakiimba kwenye moja ya mikutano ya kampeni iliyokuwa ikifanyika Wilaya ya Newala. |
|
Bi. Samia Suluhu (kushoto) akizungumza na mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia. |
|
Kulia ni Mathias
Chikawe (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani
(kulia) wakijadiliana jambo kwenye moja ya mikutano ya kampeni. |
No comments:
Post a Comment