Michel Kafando (katikati) akizungukwa na Marais Boni Yayi na Macky Sall, Jumamosi Septemba 19, 2015.
Na RFI
Baada ya
kukutana na Rais Michel Kafando, akiambatana na Rais wa Benin Boni Yayi,
Rais wa Senegal ametoa taarifa kuhusu hali inayoendelea nchini Burkina
Faso, siku mbili baada ya mapinduzi ya jenerali Gilbert Diendéré. Kwa
mujibu wa Macky Sall, njia kuondokana na mgogoro huo imeanzishwa na
inaweza kutangazwa Jumamosi hii.
"
Nimekuja na Rais Boni Yayi kumtembelea Rais Kafando. Kama mnavyonajua,
tuliomba kuachiliwa kwake mara baada ya tukio la Jumatano 16. Jenerali
Diendéré alituhakikishia kuwa ataterkeleza ombi letu. Kwa kweli tumekuja
kumuona sisi wenyewe ili kuhakikisha ukweli huo. Tummezungumza kwa kina
na Rais Michel Kafando kuhusu hali hii, vilevile kuhusu hatua za
dharura zinasopaswa kutekelezwa kwa ajili ya kurudi katika hali ya
kawaida ", amesema Rais Macky Sall.
" Kwenda katika uchaguzi mapema iwezekanavyo "
Sasa hivi
tutampokea jenerali Diendéré, na hapo itakuwa mwisho wa mazungumzo.
Tangu Ijumaa wiki hii, mlifuatilia kama sisi, pande zote zilisikilizwa,
tuna plani ambayo tumeanzisha, ni matumaini yetu kwamba ifikapo mwishoni
mwa alasiri, tunaweza kuwa wazi zaidiikiwa ni pamoja na wananchi wa
Burkina Faso, wanasiasa kutoka tabaka mbalimbali, vyama vua kiraia,
Umoja wa Mataifa, ECOWAS na jumuiya ya kimataifa, tunaweza kusaidia hii
kuondokana na hali hii ngumu, na kuendelea na mchakato wake wa mpito na
kwenda kwenye uchaguzi mapema iwezekanavyo, "amesema Macky Sall katika
mkutano na vyombo vya habari kuhusu hali inayoendelea nchini Burkina
Faso.
Aidha,
jeshi la kawaida la nchi hiyo limetoka katika ukimya wake. Mkuu wa
majeshi ametoa tangazo Jumamosi lenye uangalifu, ambapo amesema jeshi la
Burkina Faso haliungi mkono mapinduzi ya kijeshi na kuwa linajitenga na
uamzi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP). Jenerali Pingrenoma Zagre
amekumbusha kwamba jeshi linaungana na wananchi pamoja na maandili ya
taifa. Pia amelaani vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya raia.
Amehakikisha kuwa jeshi katika masaa ya kwanza ya mgogoro huo,
lilijikubalisha pamoja na wadau wa kitaifa na kimataifa katika kutafuta
ufumbuzi kwa ajili ya amani na usalama.
Usiku wa
Ijumaa kuamkia Jumamosi ulikua mfupi, lakini "mazungumzo" hatua kwa
hatua yameanzishwa Jumamosi asubuhi Septemba 19, amearifu mwandishi wetu
ambaye yuko katika mji wa Ouagadougou, Guillaume Thibault, akiongeza
kuwa shughuli za kidiplomasia zimeendelea kuongezeka katika chumba cha
hoteli Laico Ouaga ambapo Macky Sall amefikia. Thomas Boni Yayi
aliwasili katika hoteli hiyo wakati wa mchana Jumamosi mwishoni mwa huma
hili. Akiwa ameghadhabishwa na hali inayoendelea nchini Burkina Faso,
yayi Boni ameungana na mwenzake wa Senegal katika mashauriano hayo.
Viongozi
hao wawili kisha walirejea katika hoteli hiyo kuendela na mazungumzo,
ambapo walishiriki tangu saa 3:30 wanasiasa vigogo kutoka vyama
mbalimbali, na hasa wa wapinzani wa Blaise Compaoré. Miongoni mwa
waliokuwepo ni Ablassé Ouedraogo, Bénéwendé Sankara, Roch Marc Christian
Kaboré, Saran Sérémé na Zéphirin Diabré. Wote walikuwa wagombea katika
uchaguzi wa rais ulipangwa kufanyika mapema Oktoba, na wote walilaani
jaribio la mapinduzi ya kijeshi, na wameendelea kulaani jaribio hilo
mbele ya wapatanishi.
Wakati
huo huo, maandamano yameendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali
nchini Burkina Faso, ambapo watu 10 wanaarifiwa kuuawa na wengine 108
wamejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment