Bendera ya Palestina
Baraza
kuu la Umoja wa mataifa limepiga kura muswada kuipa fursa ya kipekee na
kutoa baraka zake kuiruhusu bendera ya Palestina kupepea mbele ya
majengo ya Umoja wa Mataifa .
Chini ya
azimio hilo ambalo yalilopitishwa, bendera za mataifa mawili ambayo si
mataifa kamili ambayo ni watazamaji wa umoja huo Palestina na Holy See
,sasa watakuwa na ruhusa ya kupeperusha bendera sambamba na nchi
wanachama.
Muwakilishi
wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansour,amesema kwamba
tukio hilo ni hatua kubwa kuimarisha heshima ya nchi yake .
Lakini
Israel imesema hatua hayo imeshusha hadhi ya umoja huo na kusisitiza
kwamba njia pekee kwa Palestina kupata hazi ya kuwa taifa huru ni
kupitia meza ya mazungumzo ya ana kwa ana.
No comments:
Post a Comment