Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba
wapata mafunzo ya kuripoti habari za Uchaguzi kupitia Mahojiano na
Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wananchi, wakati wa kuripoti habari za
Uchaguzi Mkuu Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi October
2015, Wakimsikiliza Mkufunzi wa Mafunzo hayo hayuko pichani, Bi Lilian
Timbuka, kutoka MCT/BBC,akiwasilisha Mada mbili za Jinsi ya Kujiandaa
katika Kufanya Mahojiano na Viongozi wa Vyama vya Siasa na Usalama wa
Kuripoti Habari za Uchaguzi Zanzibar. Mafunzo hayo yamefanyika katika
ukumbi wa hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba.Mafunzo hayo yameandaliwa na
MCT kwa kushirikiana na BBC kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuripoti
habari za Uchaguzi Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wakiwa katika
mafunzo hayo ya kuripoti habari za mahojiano na Usalama wao katika
Kipindi cha Uchaguzi yalioandaliwa na MCT na BBC Kisiwani Pemba.
Waandishi wakiwa makini wakifuatilia
Mada iliokuwa ikiwakilishwa na Muhusika wakati wa mafunzo yao ya Siku
Tatu ya kuripoti habari za Uchaguzi Zanzibar, yalioandaliwa na Baraza la
Habari Tanzania na Shirika la Utangazaji la BBC, kuwajengea uwezo
waandishi katika kazi yao ya kuripoti habari hizo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Ndg Ali Bakari
akichangia mada wakati wa mafunzo hayo. kwa waandishi yaliofanyika
kisiwani Pemba katika ukumbi wa hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba.
Baadhi ya waandishi wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwandishi mkongwe kisiwani Pemba Ndg
Hatibu Mjaja akichangia kuhusiana na waandishi kujifunza na kujituma
katika kazi yao hasa wanapofanya mahojiano na viongozi wajaribu kuwa na
kumbukumbu na jitihada binafsi.
Mwandishi wa habari wa Shirika la
Utangazaji la Zanzibar ZBC Bi, Nasra Mohammed akichangia mada kuhusiana
na muandishi kujiandaa wakati wa kufanya mahojiano na muhusika kuandaa
maswali yake na kujiamini wakati wa kazi hiyo ili kuweza kwenda sambamba
wakati wa mahojiano hayo kuepusha majibu ya ndio na hapana.
Programu Ofisa wa Baraza la Habari
Tanzania kituo cha Zanzibar Bi Shifaa Hassan akifuatilia michango
iliokuwa ikiwasilishwa na Waandishi wa Habari wakati wa mafunzo hayo ya
kuripoti habari za Uchaguzi, Mafunzo hayo yameandaliwa na MCT na BBC
kuwajengea uwezo waandishi kuripoti vizuri habari za uchaguzi bila ya
kuleta sitofahamu kwa Wananchi wakati wa kipindi hicho mafunzo hayo
yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba.na
kuwashirikisha waandishi wa Vyombo vya Serikali na Binafsi.
No comments:
Post a Comment