Muonekano
wa haiba ya uwanja wa Kufurahishia Watoto wa ZSSF-Umoja Amusement Park
uliopo Tibirinzi Chake Chake Pemba unavyoonekana kwa juu.
Baadhi
ya Pembea zilizomo ndani ya uwanja wa Kufurahishia Watoto wa ZSSF-Umoja
Amusement Park uliopo Tibirinzi Chake Chake Pemba ambazo zitakuwa
zikitoa huduma kwa wananchi wakati wa sherehe mbali mbali.
Baadhi
ya Pembea zilizomo ndani ya uwanja wa Kufurahishia Watoto wa ZSSF-Umoja
Amusement Park uliopo Tibirinzi Chake Chake Pemba ambazo zitakuwa
zikitoa huduma kwa wananchi wakati wa sherehe mbali mbali.
Baadhi
ya Pembea zilizomo ndani ya uwanja wa Kufurahishia Watoto wa ZSSF-Umoja
Amusement Park uliopo Tibirinzi Chake Chake Pemba ambazo zitakuwa
zikitoa huduma kwa wananchi wakati wa sherehe mbali mbali.
Meneja
Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {
ZSSF } Ndugu Khalifa Muumin Hilal akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif aliyefika kwenye kiwanja hicho kukagua hatua
iliyofikiwa baada ya kukamilika ujenzi wake.
Ndugu
Hilal akimueleza Balozi Seif mfumo mzima wa huduma za Umeme wa Janareta
inayoanza kutumika ndani ya sekunde tatu tuu endapo umeme wa kawaida
unapozimika ghafla katika uwanja huo bila ya kuathiri Pembea.
Wafanyakazi
wa Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi wakiwa katika majaribio ya
Vigari vitakavyotoa huduma kwenye uwanja huo ikiwa ni moja ya sehemu
inayowavutia watoto.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaagiza
wafanyakazi wa uwanja wa kufurahishia watoto Tibirinzi kufanya kazi zao
kwa upendo na unyenyekevu wakati wanapowahudumia watoto.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza wafanyakazi
wa Kiwanja cha kufurahishia Watoto cha ZSSF - Umoja Amusement Park
kiliopo Tibirinzi Chake chake Pemba kuwa waangalifu wakati wanapo
hudumia Watoto wadogo kwenye sherehe zenye mjumuiko wa watu wengi
kiwanjani hapo.
Alisema
uangalifu wa watendaji hao ndio njia pekee itakayosaidia kuwatoa hofu
Wazazi na Walezi pamoja na kuwapa upendo na faraja watoto wanaoamua
kupata huduma za burdani na michezo mbali mbali kwenye kiwanja hicho.
Balozi
Seif alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi kukagua hatua ya
Kiwanja hicho kilichozinduliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein ambacho kiko
tayari kuanza kutoa huduma katika siku za Mapumziko, sherehe za Iddi
pamoja na zile za kitaifa.
Balozi
Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Taasisi zake za
Umma mfano mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } imeamua kujenga
miundo mbinu katika maeneo ya wazi itakayowapa fursa Watoto wa Taifa
hili kupata sehemu za burdani na mapumziko baada ya harakati zao za
Kimasomo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar { ZSSF } kwa juhudi uliochukuwa wa kujenga Viwanja vya
michezo na Burdani Unguja n a Pemba kwa lengo la kukidhi haki za Watoto
hapa Nchini.
Aliwataka
wafanyakazi wa Uwanja huo kuwa waangalifu katika uendeshaji wa vyombo
mbali mbali kama Pembea vilivyomo ndani ya uwanja huo ili viweze kumudu
kwa kipindi kirefu ili kurejesha gharama ya fedha zilizotumika katika
ujenzi wa miradi hiyo.
Alifahamisha
kwamba ni vyema kwa watendaji hao kuhakikisha kwamba wanaimarisha
ushirikiano wa karibu kati yao na Uongozi husika sambamba na kutoa
Taarifa mapema pale inapotokezewa hitilafu miongoni mwa vyombo
wanavyovihudumia kama Pembea.
Mapema
Meneja Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar { ZSSF } Ndugu Khalifa Muumin Hilal alimueleza Balozi Seif
kwamba kazi iliyopo hivi sasa katika kiwanja hicho cha Tibirinzi ni
kuwapatia mafunzo watendaji wa Kiwanja hicho ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa uhakika na uelewa mpana.
Nd.
Muumin alisema wakati mafunzo hayo yakiendelea huduma za michezo na
Burdani kwenye kiwanja hicho zimeanza kwa siku za mapumziko za Jumamosi
na Jumapili na zitaendelea kama kawaida kwenye sherehe za Siku Kiuu za
Kidini pamoja na zile za Kitaifa.
Meneja
Mipango, Uwekezaji na Utafiti huyo wa ZSSF alifahamisha kwamba ipo
changamoto kubwa ya mazingira ya hali ya hewa inayoizunguuka sehemu hiyo
inayoonyesha muelekeo wa kusababisha kufanya kutu kwa baadhi ya vyuma
vya Pembea za Kiwanja hicho.
Alieleza
kuwa Uongozi kupitia Wahandisi wa Kiwanja hicho watalazimika kuwa
makini wakati wote katika kuvifanyia matengenezo vifaa hivyo kwa kupata
rangi ili viweze kutumika kwa muda mrefu.
Kiwanja
cha kufurahishia Watoto cha ZSSF - Umoja Amusement Park kiliopo
Tibirinzi Chake chake Pemba kilichojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Mazrui
Building Construction Limited kimegharimu Jumla ya Shilingi Bilioni
Saba za Kitanzania.
Zaidi
ya watu 12,000 wanaweza kuhudumiwa kwa wakati mmoja kwenye kiwanja
hicho kinachotarajiwa kurejesha gharama za fedha zilizotumika katika
kipindi cha miaka 12 ijayo.
No comments:
Post a Comment