Mwenyekiti
wa stand united Amani Vicent (kushoto) akibadilishana mkataba wa
udhamini wa timu hiyo na Makamu wa rais wa ACACIA anaeshugulikia masuala
ya Kampuni, Deo Mwanyika mara baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka
miwili na kampuni hiyo.
Baadhi ya
wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa
ligi kuu ya Vodacom mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali na
wadhamini wao kampuni ya ACACIA.
Baadhi ya
wachezaji wa Stend United wakiwa na baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa
dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Acacia ambao ni wadhamini
wa timu hiyo muda mfupi mara baada ya kuzindua rasmi jezi za timu hiyo
zitakazotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza
tarehe 12.09.2015.(P.T)
Baadhi ya
wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa
ligi kuu ya Vodacom wakati walipokuwa wakizionyesha kwa Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(Hayupo pichani wakati wa utiaji saini wa
mkataba wa timu hiyo na kampuni ya ACACIA.
Baadhi ya
Viongozi wa Acacia kutoka kulia ni Alex Lugendo (Meneja wa Uhusiano na
Serikali wa ACACIA), Elias Kastra – (Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa
Bulyanhulu)na Nector Foya - (Meneja wa Mawasiliano wa ACACIA)
wakifuatilia mchezo kati ya Stend United na Olympic Stars ya Burundi
Mchezo uliopigwa katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Baadhi ya
washabiki wa Stend United waliohudhuria wakati wa uzinduzi wa jezi mpya
za timu hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kusherekea udhamini wao na kampuni
ya Uchimbaji wa madini ya ACACIA.
Wachezaji
wa Stend United wakionyesha jezi yao itakayokuwa ikitumika kwa michezo
ya uwanja wa nyumbani na ile ya ugenini wakati wa msimu wa ligi kuu ya
Vodacom.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazo zitumia katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom.
RC wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akipokea jezi ya timu ya stend United kutoka kwa makamu wa rais wa ACACI, Deo Mwanyika.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Mguu mkoa wa Shinyanga Benasta Lugola akipokea
jezi ya timu ya stend United kutoka kwa makamu wa rais wa ACACI, Deo
Mwanyika.
Mashabiki wa Stend United waliojitokeza kusherekea udhamini wa timu yao katika uwanja wa Kambarage.
Wachezaji wa Stend United wakifanya mazoezi mepesi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo.
Timu za
Olympic Stars yenye jezi ya bluu na timu ya Stand united yenye jezi ya
rangi ya dhahabu zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo wao wa kirafiki.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na Kapteini wa timu ya Olympic Stars ya Burundi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisalimiana na kapteni wa timu ya Stand United Nassoro Masoud “CHORO”
Makamu wa rais wa Acacia
anaeshughulikia masuala ya Kampuni Deo Mwanyika akisalimiana na kapteni
wa timu ya Stand United Nassoro Masoud “CHORO” wakati timu hiyo
ilipoumana na Olympic Stars ya Burundi.
Kikosi
cha Stend United Kilichoshiriki mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu
ya Olympic Stars ya Burundi katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Mchezo huo uliisha kwa ushindi kwa timu ya Stend United Kushinda 1-0.
Kikosi cha Olympic Stars cha nchini Burundi kilichochuana vikali na Stend United ya Shinyanga Tanzania.
Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka
miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya
kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi
katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa
katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita
2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.
Udhamini
wa ACACIA katika misimu hii miwili ya ligi kuu itasaidia katika kuifanya
timu ya Stand United iweze kufanya vizuri katika michezo yake, pamoja
na kusaidia katika kuboresha programu mbalimbali za timu na kuendeleza
vipaji pamoja na masuala ya Utawala.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo Makamu wa rais wa Acacia aneshughulikia masuala ya
kampuni, Deo Mwanyika, amesema “Kwa takriban mwaka mmoja, tumekua
tukifanya kazi pamoja na Stand United. Kwa muda huo tulianzisha mchakato
wa kutambua namna nzuri ya kuboresha ushirikiano wetu ili kunufaisha
watu wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bwana Deo
amesema Msimu uliopita uliwapatia fursa nzuri ya kushuhudia uwezo wa
timu hiyo hasa ukizingatia ilikua mara yao ya kwanza kushiriki ligi kuu,
“Baada ya tathmini ya kina, tunadhani huu ni muda muafaka wa sisi
kusaini makubaliano au mkataba wa kuidhamini na kufanya kazi pamoja ya
kuikuza timu hii ya nyumbani maarufu kama “Chama la wana”.
Hivyo,
Leo, Acacia tunasaini mkataba na timu ya Stand United kwa udhamini wa
misimu miwili ya ligi kuu, wenye thamani ya Shilingi bilioni moja.
Udhamini huu unajuamuisha shughuli za uendeshaji wa timu, kuboresha
uongozi na kukuza vipaji.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent, amesema udhamini
huo wa miaka miwili utakuwa chachu kwa timu yake kufanya vizuri katika
ligi kuu, “Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi ya nane na kipindi
hicho hatukuwa na fedha ya kutosha kuendesha timu, lakini kwa udhamini
tulioupata kutoka kwa ndugu zetu wa Acacia vijana wetu safari hii
watafanya vizuri zaidi.
Kampuni
ya Acacia ni kampuni inayoongoza kwa shughuli za uchimbaji wa madini
hapa Tanzania huku ikiwa na Migodi mitatu katika kanda ya ziwa, kupitia
mradi wa “Acacia Maendeleo Fund” ambao ndio pia umetoa udhamini wa timu
ya Stend umekuwa pia ukitekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa
Jamii hapa nchi huku kampuni hiyo ikieleza kuwa dhamira yake ni
kuendelea kufanya kazi na Jamii zinazowazunguka katika kuwaletea
Maendeleo wenyeji.
No comments:
Post a Comment