Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora.
Jovina Bujulu-MAELEZO
WATANZANIA theluthi mbili hawana ufahamu wa kutosha kuhusu namna Bima inavyofanya kazi nchini hasa Bima ya Maisha na Mali.
Hayo
yamesemwa na Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora alipokuwa
akifunga mafunzo ya wiki ya huduma kifedha na uwekezaji mwishoni mwa
wiki jijini Dar es salaam.
Kamuzora aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kueneza ujuzi na ufahamu waliopata ili wananchi walio wengi waweze kunufaika na huduma za bima nchini.
“Ninawaomba
muwe mabalozi wazuri wa kueneza ufahamu juu ya faida za Bima kwa ndugu,
jamaa na marafiki ambayo ni mojawapo ya mbinu za kujilinda kimaisha na
kujikwamua katika umasikini”. Alisema Kamuzora.
Kamuzora
alisema kuwa kwa upande wao kama waratibu wa huduma za Bima nchini
wanao wajibu wa kuendelea kujenga mazingira ambayo ni rafiki na wezeshi
kwa watoa huduma ya Bima ili waendelee kuwa wabunifu katika kufikisha
huduma hiyo kwa Watanzania wenye uwezo mkubwa na mdogo.
Aidha,
Bw. Kamuzora alisema kuwa mpango wa Taifa wa huduma Jumuishi za kifedha
nchini unalenga kuwafikia watu wazima asilimia 50 wanaotumia huduma
rasmi za kifedha ifikapo mwaka 2016.
Ili
kufanikisha mpango huo, Bw. Kamuzora alitoa wito kwa taasisi za kifedha
na za utafiti wa sayansi kuendelea kushirikiana na mamlaka ya Bima
kuona namna ya kuendeleaza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya
kuwapatia wananchi fursa ya kupata huduma za Bima ili kulinda mali na
maisha ya Watanzania waliowengi.
Hadi
sasa nchini, takwimu zinaonyesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu
za mkononi nchini wanatumia huduma za fedha za simu ziliongeza ndugu
Kamuzora.
Mafunzo
ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yalipambwa kwa kauli mbiu
inayosema “Maisha ni Duni Bila Bima” yaliwahusisha wajariamali, benki,
na kampuni za Bima yalidhaminiwa na kampuni ya NUEBRAND na Shirika la
PESCODE.
No comments:
Post a Comment