Wananchi
wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga
barabara baada ya Wanafunzi wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi
na kupelekea kifo cha Mwanafunzi Mmoja
Akiongea
na Mtandao huu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jaffary
Mohammed amesema baada ya tukio hilo Wanachi walifunga barabara kutokana
na hasira ya tukio lakini jeshi la Polisi limetuliza hali na
linamshikilia Dereva wa gari hilo kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda
Jaffary ameongeza kuwa katika tukio hilo Mwanafunzi aliejeruhiwa
amelazwa katika hospitali ya Tumbi na mwili wa marehemu upo mochwari
katika hosptali hiyo.
Aidha
Jaffari ameongeza kuwa kwa sasa hali ya kiusalama imetulia baada ya
jeshi la polisi kutuliza hali iliyojitokeza huku akiwataka wananchi
kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yale wafuate sheria.
Katika
hatua nyingine amewataka madereva wafate sheria za barabarani kwa
kufuata alama zilizowekwa pamoja na kupunguza mwendo katika maeneo ya
watu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment