Licha ya mtaa wa
Mbweni JKT, jijini Dar es Salaam kujengwa majumba ya kifahari na
kupatikana pia nyumba za viongozi mbalimbali wa serikali, miundo mbinu
yake, hususan daraja linalojengwa katika eneo hilo ili kuwafanya
wananchi wapite kwa urahisi kusua sua. Kwa miaka kadhaa sasa ujenzi wa
daraja hilo umesimama.
Pichani ni gari la mwananchi na mkazi wa eneo hilo akipta kwenye maji ambayo mara kadhaa hujikuta wamesimama kwa saa kadhaa, hususan kama eneo hilo litajaa baada ya eneo hilo kujaa maji yanayotoka baharini.
Hali hiyo si tu inakwamisha maendeleo, pia ni hatari kwa usalama wa wananchi kwenye eneo hilo. Wananchi wengi wameonekana kuichoka hali hiyo na kuiomba serikali kulifanyia kazi daraja hilo ili kuwafanya wananchi waingie na kutoka bila usumbufu wowote kama unaotokea wakati huu.

Kambi
ya JKT Mbweni ikiwa tulii. Ujenzi wa daraja hilo umekwama. Wananchi
hawajui ujenzi huo umekwamia wapi. Baadhi ya wananchi waliozungumza na
mtandao huu walimuomba Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda na
Mkurugenzi wake kuangalia namna gani mradi huo umesimama kwa miaka
mitatu sasa.
Linaloonekana nyuma ya
kibao cha tangazo la Halmashauri ni daraja linalojengwa kwenye eneo la
Mbweni JKT ambalo hata hivyo limesimama na kuleta adha kubwa kwa wakazi
na wananchi wa eneo hilo kwa miaka mitatu sasa. Wananchi hao wameendelea
kutaabika hasa sehemu hiyo inavyopokea maji mengi kutoka baharini kila
wakati.
No comments:
Post a Comment