Mkurugenzi
wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani
iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada
katika semina hiyo leo ofisi za WLF.
BAADHI
ya wanahabari wa mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam wamepewa
mafunzo juu ya taarifa za uzazi na afya ya mama na mtoto ili waweze
kuelimisha zaidi jamii kupitia mitandao yao dhidi ya taarifa hizo.
Akizungumza
wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza
Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke
Mwakatundu alisema taasisi yake imeamua kutoa mafunzo hayo kwa
wanahabari hao ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii
kupitia mitandao yao juu ya umuhimu wa kupambana na vifo vya mama na
mtoto vinavyoendelea kutokea kila uchao.
Alisema
kazi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto si jukumu la madaktari au
hospitali pekee lakini jukumu la jamii nzima kukabiliana na huduma hiyo,
alisema vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii inakilasababu za
kuonesha mapungufu na kueleza changamoto katika huduma za afya
zinazotolewa kwa lengo la kuboresha zaidi huduma hizo.
Alisema
tatizo la elimu ya afya ya uzazi ni kubwa nchini kwani takwimu
zinaonesha kwa kila saa moja kuna mama anayepoteza maisha kutokana na
matatizo ya uzaziSerikali. “…Kila siku kuna akinamama takribani 24
wanapoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi nchini,” alisema Dk.
Mwakatundu.
Awali
akizungumzia hali halisi ya uzazi wa mpango nchi, Meneja Mawasiliano wa
WLF, Victoria Marijani alisema kuna faida kuwa ya kuzingatia Uzazi wa
Mpango kwani ni uwekezaji wenye faida na endelevu ambao unachangia
kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 44.
Aliongeza kuwa uwekezaji huo wa ziada katika afya, elimu, usawa wa
kijinsia na uwepo wa sera wezeshi za kiuchumi vitaiwezesha nchi kupata
manufaa yatokanayo na ukuaji wa haraka wa uchumi.
Alisema
familia zinazotumia uzazi wa mpango zinakuwa na uwezo wa kuwatimizia
watoto mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu, mavazi, huduma za afya
na makazi.
“…Atapata muda wa kushiriki katika shughuli za jamii, Atamudu kujiwekea akiba, Atakuwa na amani na upendo kwa familia yake.
Alisema
kiwango kikubwa cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 (vifo 81 kwa
vizazi hai 1000) Kiwango kidogo cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi
wa mpango (Asilimia 27). Wastani wa utumiaji wa njia za kisasa za uzazi
wa mpango hapa nchini bado ni mdogo. Ni asilimia 27 tu ya wanawake walio
kwenye umri wa kuzaa ndio wanaotumia njia za kisasa za Uzazi wa Mpango.
No comments:
Post a Comment