KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom leo imetiliana saini na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF mkataba wa kuendelea kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kipindi kingine cha miaka mitatu. Kampuni hiyo imeendelea kuidhamini ligi hii baada ya kuidhamini kwa miaka minane mfululizo iliyopita.
Mkataba huo umetiwa saini kwenye mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Makao Makuu ya Vodacom yaliyopo Mlimani City Jijini Dar es Salaam.



No comments:
Post a Comment