Taarifa rasmi kutoka TCRA ni kwamba Sheria ya Matumizi ya Mitandao itaanza rasmi September 2015 Tanzania, hali iliyopo sasahivi kumekuwa na ishu ya uzushi na uvumi mwingi sana mitandaoni, wapo ambao wanaendesha account kwenye Mitandao ya Kijamii na wanatumia majina ya watu wengine, na bado wametumia kivuli hichohicho kueneza taarifa za uongo, kama ukifanya hivyo China hauko kwenye upande salama hata kidogo !!
Kuna mlipuko ambao umetokea Jiji la Tianjin China siku chache zilizopita, watu zaidi ya 50 wamefariki na wengine zaidi ya 700 walijeruhiwa.
Moshi ukiendelea kufuka baada ya mlipuko kutokea Jiji la Tianjin, China.
Baada ya tukio hilo kuna watu ambao walianza kusambaza uzushi kwenye mitandao kwamba kuna milipuko mingine imetokea, watu wengine wamefariki na kujeruhuiwa !! Haikuwa kweli, Serikali ya China haikuwaacha waliozusha huu uongo, account 360 za watu kwenye Mitandao ya Kijamii zimefungiwa.
Kwenye account zilizofungwa zipo pia nyingine ambazo watu walianzisha wakidanganya watu kwamba wao ni ndugu na jamaa wa waathirika wa mlipuko huo kwa hiyo walikuwa wanahitaji kuchangiwa misaada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment