UJERUMANI YAISAIDIA SERIKALI YA TANZANIA SH. BILIONI 39.1 - LEKULE

Breaking

13 Aug 2015

UJERUMANI YAISAIDIA SERIKALI YA TANZANIA SH. BILIONI 39.1

lil1
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam.
lil2
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kulia) akisaini hati ya makubaliano katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke.
lil3
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, ujumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam.
lil4
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam.
lil5
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili.
lil6
Baadhi ya wajumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (hayupo pichani) alipokuwa anaongea wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam.
lil7
Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili leo alhamisi (Agosti 13, 2015) Jijini Dar Es Salaam.

Serikali ya Tanzania na Ujerumani zimetiliana saini mikataba miwili ya misaada yenye thamani ya jumla ya Sh. Bilioni 39. 1 ambazo ni sawa na Euro milioni 17 kusaidia sekta mbalimbali nchini.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke ili kuleta mafanikio na maendeleo katika.
Sekta zitakazonufaika na msaada huo uliotolewa na Serikali ya Ujerumani ni pamoja na sekta ya afya, maji na maliasili.
Aidha, Dkt. Likwelile amemhakikishia Balozi Kochanke na ujumbe wake kuwa msaada walioipa Serikali utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta ufanisi na kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuchangia katika kuboresha uchumi nchini.
Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke amesema kuwa serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Zaidi ya hayo, serikali hizo mbili zimesaini mkataba wenye thamani ya Euro milioni 10 ambazo ni sawa na bilioni 23 za kitanzania kuisaidia usimamizi wa hifadhi ya taifa ya Selous.


No comments: