Kufuatia
tatizo la kiufundi la umeme katika uwanja wa Ndege wa Mwanza ambalo
lilisababisha ndege za kampuni ya Fastjet kukatisha safari zake zote za
usiku kuepuka kuhatarisha maisha ya abiria na wafanyakazi, tunapenda
kuwashukuru wateja wetu wote kwa ushirikiano wao na uvumilivu
waliotuonyesha na tunawaomba wawasiliane nasi ili kupata maelezo zaidi
juu ya safari zao.
Wakati
mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ikiendelea kufanya juhudi za
kutatua tatizo hili, safari zetu za usiku za kuingia na kutoka jijini
Mwanza zinaendelea kusitishwa na tutawapa maelezo zaidi mapema
iwezekavyo huduma zetu zitakaporejea.
Tunawataarifu
kuwa safari zetu za mchana zinaendelea kikamilifu na wateja wa Fastjet
wana haki ya kuahirisha safari zao zilizositishwa au kupata tiketi
nyingine ndani ya siku saba kuanzia leo au kudai pesa kwa tiketi zozote
ambazo hazikutumika.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba, usalama wao ndio wajibu wetu mkubwa!
Habari zaidi zitakuwa zikitolewa pale zinapopatikana.
No comments:
Post a Comment