Japan
inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la
Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima, na siku tatu baadae mjini
Nagasaki.
Shambulio hilo la bomu lililodondoshwa katika mji wa Hiroshima liliwaua maelfu ya raia. Ilikua tarehe 6 Agosti mwaka 1945.
Wakati
bomu hilo la atomiki liliporushwa na ndege ya kivita ya Marekani B-29
Enola Bay, ambayo ilikua ikiruka kwenye umbali wa juu wa mita 600 kutoka
ardhini katika anga la mji wa Hiroshima, wakaazi 300,000 wa mji huo
walijikuta hawana makaazi kufuatia mlipuko wa bomu hilo.
Takriban
watu laki moja na arobaini walipoteza maisha. Watu elfu sabini na tano
walifariki papo hapo baada ya ndege ya Marekani kudondosha bomu hilo la
atomiki, huku watu wengine hamsini walifariki kutokana na athari za
mionzi ya sumu, na wengine zaidi ya 200,000 walijikuta walipoteza baadhi
ya viungo vyao vya mwili, na wengi walipoteza ajira na wengine
kushindwa kufunga ndoa kutokana na ulemavu ambao waliendelea kuupata
kufuatia sumu ya bomu hilo la atomiki lililodondoshwa katika mji wa
Hiroshima.
Akilihutubia
taifa, Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kumbukumbu ya Heroshima
inaonesha jinsi gani jitihada zinatakiwa kufantwa katika kupiga vita
matumizi ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment