Hollywood, marekani
Staa wa muziki na filamu Selena Gomez amedai kuwa hajutii kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Justin Bieber kwa sababu anaamini kuwa naye ilikuwa ni sehemu ya tuisheni ya kujifunza mapenzi.
Selena
Gomez aliyasema hayo katika mahojiano na mtandao mmoja maarufu nchini
humo ambapo alikiri kutowahi kuwa kwenye penzi zito kama alilopitia
akiwa na Bieber ambapo aliongeza kuwa anaamini penzi lijalo kwake
litakuwa zuri kwa sababu ya mafunzo hayo aliyoyapata kwake.
“Bado sina mpenzi lakini naamini penzi langu lijalo litakuwa zuri na la kipekee sana kwangu kwa sababu nimejifunza mengi kupitia uhusiano wangu na Bieber. Wala sijutii kuachana naye,” alisema Selena ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka na ‘muuza sura’ anayejulikana kwa jina la Nick Jonas huku Justin Bieber akitoka na msichana anayefahamika kwa jina la Jayde Pierce.
Staa wa muziki na filamu Selena Gomez amedai kuwa hajutii kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Justin Bieber kwa sababu anaamini kuwa naye ilikuwa ni sehemu ya tuisheni ya kujifunza mapenzi.
“Bado sina mpenzi lakini naamini penzi langu lijalo litakuwa zuri na la kipekee sana kwangu kwa sababu nimejifunza mengi kupitia uhusiano wangu na Bieber. Wala sijutii kuachana naye,” alisema Selena ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka na ‘muuza sura’ anayejulikana kwa jina la Nick Jonas huku Justin Bieber akitoka na msichana anayefahamika kwa jina la Jayde Pierce.

No comments:
Post a Comment