Vikosi vya Usalama nchini Sudani
Kusini vimefunga kituo cha redio iliyokuwa ikiunga mkono mpango wa
kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.
Mamlaka
ya nchi hiyo, imekilazimisha kituo cha radio cha Free Voice South Sudan
kinachoungwa mkono na Marekani kutorusha matangazo yake siku ya
Jumanne, siku moja tu baada ya kulifungia gazeti la The Citizen.Wapatanishi wa kimataifa wamewapa rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar mpaka katikati ya mwezi Agosti kusaini makubaliano ya amani.
Kwa upande wake, rais Obama amewatuhumu viongozi hao wawili kwa kile alichokiita kusambaratisha matumaini ya taifa changa zaidi duniani.
Mpaka sasa maelfu ya vijana wameuawa na takriban watu milioni moja na nusu wamekimbia makazi yao tangu mgogoro huo ulipoanza yapata miaka miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment