Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana amewaapisha Majaji 14 akiwamo Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani Tanzania katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imebainisha kuwa Rais
Kikwete aliwateua majaji hao hivi karibuni katika mwendelezo wake wa
kuhakikisha kuwa Muhimili wa Mahakama unakuwa na raslimali watu wa
kutosha ili kuendelea kutoa haki kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.
Walioapishwa katika sherehe iliyohudhuriwa pia na Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman ni pamoja na Jaji Richard
Mziray ambaye anakuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Majaji wengine ambao wote ni Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni
Mheshimiwa Ignas Pius Kitusi, Mheshimiwa Lameck Michael Mlacha,
Mheshimiwa Wilfred Peter Dyansobera, Mheshimiwa Salima Mussa
Chikoyo, Mheshimiwa Issa Kweka Arufani, Mheshimiwa Sirilius Betran
Matupa na Mheshimiwa Julius Benedicto Malaba.
Wengine ni Mheshimiwa Victoria Lyimo Makani, Mheshimiwa Lucia Gamuya
Kairo, Mheshimiwa Rehema Joseph Kirefu, Mheshimiwa Benhaji Shaaban
Masoud, Mheshimiwa Issa John Maige na Mheshimiwa Adam Juma Mwambi.
No comments:
Post a Comment