MAJANGA mbalilmbali
nchini ambayo yamekuwa yakitokea na kushindwa kupata msaada ni
kutokana na kuwa vifaa duni vya mawasiliano ya radio.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam wa Maonyesho na Mkutano wa Mawasiliano ya Radio za Kisasa ‘Radio Call’
Naibu
Mkurugenzi wa Masafa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Libena
Denis amesema kuwa kazi kubwa na kuona mawasiliano ya radio yanakua na
hivyo TCRA lazima isimamie.
Denis
amesema kuwa kampuni ya Airsys kuleta mawasiliano ya radio za kisasa
na kuondokana na radio za kizamani ambazo kwa mabadiliko ya kitekonojia
haziwezi kuhimili.
Aidha
amesema kuwa nchi za ulaya zimekuwa zikitumia mawasiliano hayo hivyo
kuingia nchini itasaidia katika mawasiliano ya radio.
Amesema
Meneja Mkuu wa Airsys Communication Technology Ltd,Sanctus Mtsimbe
amesema mawasiliano ya matumizi ya radio yatakuwa nchini na kutoa
urahisi wa upatikanaji wa huduma na mafunzo kwa wateja.
Amesema Tanzania imepewa kuwa kanda ya Afrika Mashariki kwa kuwa na huduma ya Radio Call hivyo watumiaji watapata msaada na kuondokana na usumbufu wa kuagiza radio nje.
Balozi
wa marekani hapa nchini,Dianna Melrose akizungumza wakati wa kuzindua
mkutano wa kampuni ya Airsy katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam leo.
Afisa
mtendaji mkuu,Hans Beckers akionyesha redio call ambazo zinatengenezwa
na kampuni ya Airsy ambazo zitakuwa zikisaidia katika ulinzi katika nchi
mbalimbali ambazo zitakuwa zikisambazwa hapa nchini alionyesha redio
hizo katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es
Salaam leo.
Naibu
Mkurugenzi wa Masafa wa Mamlaka ya mawasiliano (TCRA), Libena Denis
akizungumza katika mkutano wa kuwaonyesha watanzania jinsi redio hizo
zinavyo fanya kazi katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya waliohudhulia katika mkutano.
Meneja wa mauzo wa kampuni ya Airsys,Raurent Tribout akitoa maelezo kuhusiana na mauzo ya redio kalu hizo.
Msemaji wa kampuni ya Airsys, Sanctus Mtsimbe akizungumza na waandishi wa habari leo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa mtendaji mkuu,Hans Beckers wa kampuni ya Airsy.
No comments:
Post a Comment