Polisi Wazuia Msafara wa LOWASSA Kushiriki Mazishi ya Mzee Kisumo - LEKULE

Breaking

13 Aug 2015

Polisi Wazuia Msafara wa LOWASSA Kushiriki Mazishi ya Mzee Kisumo


Polisi mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.

Vyanzo vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.

Taarifa zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.

Baada ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.
Polisi  wakiwa  tayari  kwa  lolote  baada  ya  kuzuia  msafara  wa  LOWASSA

No comments: