9:31 Mchana: Edward Lowassa akiwa na mgombea mwenza Haji Duni wanaingia kwenye viwanja vya Jangwani wakiwa kwenye gari la wazi.
9:43 Mchana: Lowassa amefika meza kuu na kuketi, meza kuu pia wamo Maalim Seif, Duni, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Salum Mwalim na wengineo.
9:48 Mchana:
Sasa ni muda wa viongozi wa dini kuomba dua, Said Riko kwa niaba ya
dini ya Kiislam anaomba dua na atafata mchungaji Gwajima kwa upande wa
dini ya kikristo kuongoza sala kwa niaba ya wakristo.
9:56 Mchana: Baada ya dua, kilichopo kwa sasa ni wimbo wa taifa
Salum Mwalimu(9:59): Tunakutana
hapa kwa sababu ya mambo mawili, jambo la kwanza kuzindua rasmi kampeni
zetu. Jambo la pili ni kuzindua ilani yetu ya uchaguzi mkuu, japokuwa
inazinduliwa na CHADEMA inaungwa mkono na vyama vyote vilivyo kwenye
UKAWA.
Imani
yenu kamwe haitapotea bura, mnaiweka mahali sahihi na sisi
tutaisimamia. Natangaza rasmi sasa mkutano wetu umezinduliwa na tusubiri
nondo zenye hoja.
Lawrence Masha:
Waheshimiwa viongozi, watanzania wenzangu, sisi sote ambao tumehama CCM
tuna akili timimu, sio wapumbavu, sio makapi. Kutokana na mambo
yaliyotutokea mimi na vijana, wale wote wanaofanya kazi katika serikali
yetu, magereza, polisi mahakama kuu, niwapongeze wote waliofata maadili
yao ya kazi lakini wapo wachache wasiofata maadili yao ya kazi.
Mabadiliko yanakuja na ndugu zangu msiogope na tarehe 25 mpige kura
tuingize serikali mpya ya UKAWA.
Mdee: Niseme
mambo machache, kwa kipindi kirefu wanawake wa nchi tumekuwa wateja wa
chama cha mapinduzi, kwa kipindi kirefu sana sisi ambao ni wahanga
kwenye huduma za afya, tunaojifungulia chini.
2010
CCM waliahidi kununua bajaji kwa ajili ya wanawake wajawazito, Kikwete
amejitengea bilioni 50 kwenda mamtoni, pesa hizo pekee zingetosha
kununulia ambulance 300, wakati ni huu, imetosha. Tumalizie kwa kupiga
kibwagizo.
Nimeambiwa niombe kura za Kawe, wanakawe mpoo, mtanipaa, asanteni sana
Mama Regina:
Wakinamama mpo! Kwangu Mungu ametenda, mimi juzi nimeongea na wanawake
wenzangu Tanzania nzima kupitia wanawake wa Dar, matatizo ya mwanamke
nayafamu japokuwa sio yote.
Nachowaomba wanawake wenzangu tushirikiane, mabadiliko haya tutayaleta sisi kwa umoja wetu. Mungu awabariki sana.
Mbowe:
Dar es Salaam Oyeee, DJ tafadhali naomba utupe utulivu. Kwa sababu ya
muda nizungumze kwa kifupi sana, ukiona hicho kidude kinaruka juu ni
mtambo wa kupigia picha. Kwa sababu ya muda niende kwenye tukio la
kuzindua Ilani. Tunazindua ilani kama CHADEMA lakini ilani hii pia ni
ilani ya CUF, NLD na NCCR.
Niwatambulishe
wagombea wetu wa ubunge kwa Dar es Salaam. (Sasa ni tukio la kukabidhi
ilani na nakala za ilani zinakabidhiwa Lowassa Lowassa, Duni na Hamad
Sharif)
Sasa
ni zoezi la kutambulisha wabunge watakaowania ubunge katika majimbo ya
Dar es Salaam kasoro majimbo mawili ya Segerea na Kigamboni yana
wagombea wawili wa UKAWA kila moja
Mbowe:
Majimbo yote tunasema tunasimamisha mgombea mmoja, lakini majimbo
mawili bado taratibu hazijakamilika lakini naamini yatakamilika
Wanaowania ubunge Dar es Salaam
Mtulia
Said, Mwita Mwaitabe, Said Kubenea(Ubungo) Halima Mdee(Kawe) Julius
Mtatiro(Segerea ushind Shaaban Nkumbi Kigamboni John Mnyika Kibamba
Naotrapia (CHADEMA jimbo la Segerea) Kondo (Mbagala) na Asanali (Lofa wa
Ilala)
Makaidi(NLD): Zamani
mimi nilikuwa mwanamichezo mpiga mpira na mwenyekiti wa SImba kwa miaka
mingi, Simba huu ndio mwaka wao na Yanga, mpira hauwezi kuwa mzuri kama
siasa ni mbaya, tuhakikishe tunachague sera nzuri ya UKAWA, hivi
haiwezekani kutengeneza picha yenye sura ya Lowassa, sura yake nzuri
yenye nywele nyeupe.
Miaka 50 iliyoputa nilisema ipo siku TANU itapata jambajamba, mwaka huu TANU na CCM yake imepata jambajamba.
Taslima(CUF):
Kinachosemwa hapa ni mabadiliko, tunatoka mahali pabaya, tunaingia
mahali pazuri. Mabadiliko hayazuiliki isipokuwa waliodhani mabadiliko
yanaweza kuletwa na CCM peke yake, hayo mawazo wayaondoe.
Mbatia(NCCR):
Lowassa amesomea digrii ya pili Uingereza, degree ya maendeleo.
Serikali atakayoiunda tutashirikiana kwa pamoja. Lowassa tunahakikishia
umma wa watanzania utakulinda. Biblia inasema pasipo na kuni hakuna
moto, pasipo na uchochezi hakuna vita.
Wao
wanachochea vurugu, sisi tunaleta matumaini yenye heri kwa watanzania,
matusi na uchochezi huo kuna maandiko kwenye bibilia yanasema heri
kijana masikini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambae hasikii
tena maonyo na Mtume amesema ukiona uovu kemea, ukiona huwezi basi weka
chuki. (Anamalizi kwa kuimba wimbo)
Mbowe(CHADEMA):
Asanteni sana Dar es Salaam, nitaongea kifupi sana kwa sababu ya muda,
leo hii tunazindua rasmi kampeni za mgombea wa Urais, mgombea mwenza na
wagombea wote wa UKAWA kwa nchi nzima.
Tunataka
mabadiliko haya yakalete maisha mapya, nawashukuru sana viongozi
viongozi wenzangu na zaidi waliopata ujasiri wa kuondoka CCM wakiongozwa
na Lowassa, akafatiwa na mzee Sumaye na wengine ambao sitawataja kwa
sababu ya muda.
Mzee
Warioba umasikini sio sifa, wala sisi katika umoja wa UKAWA hatuutamani
umasikini, wakati wa kuamini viongozi masikini hapana. Tunataka
Tanzania iondoke katika umasikini kwa sababu umasikini ni laana.
Nimalizie
kusema kwa nini Lowassa, sisi tulifanya tafiti, kwa sababu taifa letu
limeendeshwa kwa propaganda kwa muda mrefu, Lowassa kwa muda wa miaka 10
amekuwa muhanga wa propaganda za CCM.
Nawashukuru
sana Dar, niwaahidi tutafanya kampeni za kistaarabu, hataibiwa mtu
simu, sadaka ya mabadiliko itafanywa katika kampeni nyingine.
Nimkaribishe mheshimiwa Sumaye.
Sumaye:
Kwa ajili ya muda nitasema kwa kifupi sana, nimetoka chama cha
mapinduzi, katibu mkuu alisema sisi ambao hatukuteuliwa hatukuwa na
maadili, mimi nasema kama kipimo cha maadili ni mheshimiwa Kinana, mimi
nitakuwa mtakatifu, CCM wamekuwa wakiongoza siasa ya chama kimoja kwa
ngozi ya vyama vingi, mmekunjika kwa miaka yote.
Tulitaka
kufanya mabadiliko kulekule, kukawa na tatizo ndani ya CCM, ukitaka
kufanya lolote wanakuzingira. Wanawajaza watanzania uoga wa usilolijua,
mkiwapa wapinzani wataharibu nchi, kila binadamu ana uoga wa asilolijua.
Lowassa
kwa kuliona hilo, kwa kuwa watanzania wanamfahamu aliona uoga wa aina
hiyo haitakuwepo, na mimi nimekuja kwa sababu hiyo. Watanzania leo elimu
yetu inashuka sana, tunashusha alama za kufaulu wanafunzi ionekane
wamefaulu wengi, pia ukienda katika afya. Tunataka tubadilishe hali
hiyo.
Leo
Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni KIkwete aliemfanya
waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai? Lakini ni
LOwassa huyuhuyu ndie aliemuingiza KIkwete Ikulu, Kwamba watanzania
wanampenda Lowassa, halina mjadala.
Mmewasikia
kwenye kampeni zao, fisadi mkubwa huyo amechukua fedha za matajiri,
Lowassa amechukua ustaarabu wa kuwajibika. Waziri anachukua mzigo ili
kumuokoa Rais na serikali yake. Asanteni sana.
Nyerere
wakati anastaafu, kwenye kikao kimoja nafikiri cha halmashauri kuu.
Alisema hajaona mtu mvumilivu kama Kawawa, alibeba mizigo aliyostahili
kubeba yeye, ndiyo kazi aliyofanya Lowassa.
Vichwa
vya treni vinavyonunuliwa, Lowassa alikuwepo? Wajenzi wa barabara nchi
hii wanaidai serikali trilioni 1.4, kudai si tatizo katika hizo bilioni
900 ni pesa za adhabu, huo si ufisadi, mbona hawasemi? Serikali hii ni
dhaifu sana na alituthibitishia katibu mkuu, mwenyewe kusema kuna
mawaziri mizigo.
Mwisho
wanalomsema nalo, Escrow Lowassa alikuwepo, kile kipande cha Lugemalira
tulijua waliokula, kile kipande cha Habinder ni nani aliekula, tangu
lini benki ikaruhusiwa kutoa cash kwa mabilioni. Wamejenga kibr,
hawajali tena maumivu ya wananchi, naomba mwaka huu msikubali,
watanzania mfurahie mabadiliko ya ndani ya vyama vingi.
Wanasema
mgonjwa, mimi nataka niwaulize, kwani Magufuli mzima? Wanaenda kufanya
nini Ulaya kama ni wazima, mtu yeyote ukishavuka miaka 50 hauwezi kuwa
wazima kwa asilimia 100, hivi Rais mkapa alipokuwa madarakani hakwenda
kufanyiwa operashi Ulaya, nchi ilidorora? Alienda akarudi akaikuta nchi
usalama.
Kwani KIkwete alivyokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa upasuaji mkubwa Markani??
Rais
si kazi ya kubeba zege Ikulu, anatakiwa kuwake timu nzuri ya kazi, yeye
ni meneja tu, naomba sana tumchague itakapofika tarehe 25 Oktoba.
Asanteni sana, nawashukuru.
Maalim Seif(11:20): Kwa sababu ya muda mimi sitaki nizungumze leo, namkaribisha babu Duni ili azungumze na nyinyi
Duni(11:21): Na mimi kwa kuzingatia muda sina haja ya kusema sena, mimi natakiwa kumsaidia Lowassa atakapokuwa Ikulu. Katika mambo ambayo yametokea kwa miaka 50 ni watanzania kuonewa, Tanzania hakuna haki, tangu 95, wanaoonewa ni wapinzani tu, wanafunguliwa kesi za jabu ajabu, kunamajitu yanayoitwa mijanja weed, kuna majitu yanaitwa zombi, huku bara TV zinazuiliwa, mazikoni hatutakiwi, G/Mboto tabu.
Unapoonea watu wanajenga chuki, pamoja na kuambiwa Tanzania ina amani haina amani, wenye amani ni wanyonge kwa ajili ya stahamala zao, tumeonewa vya kutosha, sasa tunasema basi, tunataka mageuzi.
Nini tutafanya tukiwa IKulu, Hakuna kitu muhimu kama kuwa na katiba ya wananchi wote, miaka hamsini hatujawahi kuwa na katiba yenye ridhaa kwa pande mbili. Lazima tufanye kama Afrika kusini, tutaunda tume kama ya Afrika kusini, tume ya maridhiano tusameheane na tutafunga kitabu cha uhasama mabadiliko yatakapotoka.
Mdee amekuja kuzungumza matatizo ya kina mama, umma wote hapa huu umezaliwa na mwanamke, kitu muhimu tunachohitaji kufanya ni kuwaheshimu wakina mama. Sasa ni Lowassaaa.
Tambwe Hizza: Peoples, kwanza naomba mnisamehe, mwenzanu nilienda kuongeza ulofa kwenye kiwanda cha ulofa.
Watu wazito wameamua kukiacha chama cha mapinduzi, na mimi nimeamua na wapo wengi wameogopa eti watasema ana tamaa, hivi nani hana tamaa, hata Magufuli aliacha ualimu.
Napenda sana Lowassa na Sumaye, juzi nilimuona Rais akifanya utani na bosi wake, Kikwete akiwa waziri, Sumaye alikuwa waziri mkuu, eti anasema hajamuelewa, hivi ukishindwa kumuelewa bosi wako utaweza kuwaelewa watanzania.
Mwakyembe wakati akiwa mwenyekiti wa NBC, Mkapa alipotaka kuuza benki, Mwakyembe kwa mdomo wake alisema sikubali, leo anatumiwa kuja kumchafua mheshimiwa Lowassa.
Edward Lowassa(11:41): Peoples, Bwana Yesu asifiwe, tumsifie yesu Kristo, kuna tatizo kidogo muda umeenda wasije kupata sababu ya chama ipo kwenye maandishi, kwenye tovuti ya chama.
Niwashukuru waliopita kwa kunisemea, niliahidi kampeni safi lakini wameanza lakini wakianza ndio hivyo watavyopata. Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu.
Maneno haya nimeyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa gharama ya serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha.
Tatu tumeweka umuhimu sana kwenye afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo. Wanokwenda nje ya nchi ni watu wakubwa, eneo jingine ni mawasiliano, ni muhimu sana tuwekeze.
Kwa hio jambo la kwanza nitakalofanya ni kujenga upya reli ya kati iende Kigoma na Mwanza. Tutafufua Air Tanzania, nisme mambo matatu ya mwisho.
Mashehe wa Zanzibar wako jela muda mrefu sasa, nasikia habari ya babu Seya, nimeisikia. Naelewa hisia zenu kuhusu babu Seya, Tutatumia utawala bora kuwatoa muda ukifika.

No comments:
Post a Comment