New
KOCHA wa viungo wa Simba, Dusan Momcilovic amesema
mshambuliaji raia wa Senegal, Papa Niang bado hayuko fiti, hivyo anahitaji muda
zaidi wa kufanya mazoezi.
Akizungumza
baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Boko Veterani Dusan
alisema anatarajia baada ya wiki tatu hadi tano anaweza kuzungumza uwezo wa
mchezaji huyo.
“Papa
ameanza mazoezi leo nimeona fitness yake ni ya kawaida, hivyo nahitaji
muda zaidi afanye mazoezi niweze kupima uwezo wake na tutakapokuwa Zanzibar
nitakuwa na muda zaidi wa kumfuatilia kwa karibu kwani anahitaji mazoezi ya
peke yake”, alisema Dusan.
Dusan
ambaye ni raia wa Serbia alisema wachezaji wa Simba uwezo wao upo vizuri na
watakapoanza ligi anatarajia watafanya vizuri.
Papa
Niang aliwasili jijini Dar es Salaam juzi kwa ajili ya kuanza majaribio yake ya
kujiunga na klabu ya Simba.
Endapo
Niang ataonesha kiwango cha kumvutia kocha mkuu, Dylan Kerr pamoja na benchi
zima la ufundi, huenda akapewa mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ambayo imekuwa
ikihaha kutafuta washambuliaji wa kigeni.
Niang
aliyezaliwa Desemba 5, 1988 katika mji wa Matam Senegal ana urefu wa mita 1.81.
Endapo
Niang atafanikiwa kusajiliwa Simba basi atasajiliwa kama mchezaji huru kwani
mkataba wake na Mounana CF ya Gabona ambayo ilimsajili 2014-2015
ulishamalizika.
Pia
aliwahi kuchezea timu za Al Shabab SC ya
Kuwait, FC Vostok ya Kazakhstan, FF Jaro, AC Oulu na FC OPA za Finland.
Niang
ambaye ni mdogo wa damu wa Mamadou Niang ambaye kwa sasa anamalizia soka yake
FF Jaro baada ya kuwika Ulaya na Asia alisema anafurahi kuja Tanzania na
amefurahia mazingira japo kuna tofauti kidogo.
No comments:
Post a Comment