KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wanachama waliokihama
chama hicho wamejivua nguo mbele za watu na kwamba wapinzani
wanaowachukua wanahangaika na mafuta machafu.
Aidha,
amesema aliyekuwa Mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,
Dk Milton Mahanga, alikuwa anatafuta sababu za kuihama CCM na anamtakia
kila la heri, yeye na rafiki yake, Edward Lowassa.
Nape
aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari katika
Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, alipotakiwa kueleza kuhusu
kuhama kwa Lowassa na Dk Mahanga ambao wote kwa nyakati tofauti
wamekimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Lowassa
alijitoa CCM wiki moja iliyopita baada ya kukwama uteuzi wa CCM wa kuwa
mgombea wake wa urais na kukimbilia Chadema ambako anatarajiwa kuwa
mgombea wake wa urais na kuungwa mkono na Umoja wa Vyama vinne vya
Upinzani (Ukawa).
Dk Mahanga naye alijitoa juzi baada ya kukwama katika kura za maoni jimboni Segerea. “Wanahangaika
na oil chafu. Hawa ni wale wale kama ilivyokuwa Mrema (Augustino) mwaka
1995, akabebwa kiasi cha Mwalimu Nyerere kusema mwacheni abebwa.
"Hebu jiulizeni wanaona ubaya wanapotoka, lakini mambo yakiwanyookea hawasemi, wakitoka ndio maneno mengi,” alisema Nape.
Alisema kuondoka kwa Lowassa na wengine wachache, si jambo la kwanza kutokea CCM, na pia si la ajabu wala haliwezi kuwa la mwisho huku akimtuhumu Dk Mahanga kuwa alikuwa akitafuta sababu ya kuondoka CCM.
Alisema kuondoka kwa Lowassa na wengine wachache, si jambo la kwanza kutokea CCM, na pia si la ajabu wala haliwezi kuwa la mwisho huku akimtuhumu Dk Mahanga kuwa alikuwa akitafuta sababu ya kuondoka CCM.
Akizungumzia
mchakato wake Mtama, Nape alisema kulifanyika juhudi kubwa za mafisadi
kuhakikisha anashindwa, lakini anashukuru ameshinda na kwamba endapo
atapitishwa na chama hicho kugombea ubunge, ana hakika atashinda kwani
ni mwadilifu na anayezingatia ya chama hicho ikiwamo kupiga vita rushwa.
No comments:
Post a Comment