Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake,Mh.
Dkt. Makongoro Mahanga, ametangaza kuihama CCM na kuhamia CHADEMA
kutokana na kutokuwepo Demokrasia ya Kweli ndani ya CCM.
Dr.
Mahanga ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake kwenye Jimbo la
Segerea kwa tiketi ya CCM
ametangaZA azma hiyo leo mchana baada ya rufaa yake ya kupinga ushindi
wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kipawa mama Kivela kutupiliwa mbali
na Ofisi ya CCM mkoa wa Ilala.
Duru
za Kisiasa zinasema kilichomponza Dr. Mahanga ni kitendo chake cha
yeye kuhusika katika mpango wa kumnadi Waziri mkuu wa zamani Edward
Lowassa kwenye nafasi ya Urais wa CCM, ambaye kwa sasa ametangaza
kugombea urais kupitia Chadema.
No comments:
Post a Comment