Mwanzilishi wa mtandao wa facebook Mark Zickerberg na mkewe Priscilla Chan wanatarajia mtoto wa kike.
Wawili
hao walitangaza katika ujumbe wao katika ukurasa wa facebook wa bwana
Zuckerberg, ''Priscilla na mimi tuna habari njema:''Tunatarajiwa mtoto
wa kike'', aliwaandikia takriban watu milioni 33 wanaomfuata katika
mtandao huo.Katika ujumbe wake Zuckerberg mwenye umri wa miaka 31 alifichua kwamba mkewe aliharibikiwa na mimba mara tatu hapo awali,lakini akongezea kwamba hatari ya kuharibikiwa na mimba nyengine kwa sasa iko chini sana.
Amesema kwamba wameamua kutoa tangazo hilo ili kuwapa watu wanaokabiliwa na tatizo kama hilo motisha wa kuendelea kuwa na subra.
No comments:
Post a Comment