Mke wa Dude aenda kwao - LEKULE

Breaking

3 Aug 2015

Mke wa Dude aenda kwao

Mke wa staa wa maigizo Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ anayefahamika kwa jina la Eva.
Brighton Masalu
Madai mazito! Mke wa staa wa maigizo Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ anayefahamika zaidi kwa jina la Eva wa Dude anadaiwa kwenda kwao kufuatia kuwepo kwa skendo ya kimapenzi ya mumewe akihusishwa na penzi la mwigizaji mwenzake, Ester Kiama.
Staa wa maigizo Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akimwaga ‘ubuyu’ mbele ya kijumbe wa mtandao huu, mmoja wa watu wa karibu wa wawili hao alinyetisha kwamba, ni wiki moja na siku kadhaa sasa tangu Eva  (pichani)aondoke nyumbani kwake, Jeti-Lumo, Dar na kwenda kwao (haikuelezwa wapi).
Ester Kiama
“Ninavyoongea Eva hayupo nyumbani, yuko kwao lakini Dude ana kibarua kizito cha kumbembeleza na kwamba yupo tayari kukaa mbali na Ester lakini si kumkosa Eva wake, lakini ndugu nao hawataki Eva arudi kwa Dude sasa hivi, wanataka apumzike kwanza,” alisema mtoa taarifa huyo.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya Dude na kummwagia ‘upupu’ wote ambapo alijibu kwa staili ya kuingia na kutoka kwa kile alichokiita ‘ni mambo ya kifamilia’.

“Aah, mbona mnaingilia sana mambo yangu ya ndani jamani, ni kweli Eva yuko kwa ndugu zake, lakini si kwa ubaya, kwani mtu akiolewa haruhusiwi kwenda kusalimia kwao?

“Mbona huo ugomvi ni wa siku nyingi sana? Tulishaweka mambo sawa, unajua mke wangu (Eva) ni mtu muelewa, anajua fika ukaribu wangu na Ester si kama unavyotafsiriwa na baadhi ya wambeya,” alisema Dude kisha akakata simu.



No comments: