Mcheza tenisi wa nchini Australia Nick Kyrgios ametozwa faini ya dolla za marekani elfu kumi baada ya kumtusi na kumkashifu mchezaji mwenzake Stan Wawrinka wakati wa michuano ya wazi ya Ufaransa katika mji wa Montreal mapema wiki hii.
Kyrgios baadae aliomba radhi kwa kile alichokiitaa kuwa ni ''kupitiwa'' kwenye maneno yake ambapo alimzungumzia Wawrinka, akisema mchumba wake alikuwa na uhusiano na mwanamichezo mwingine wa Australia.
Kyrgios ambaye ni mshindi wa robo tatu ya dola milioni moja za kimarekani katika fedha za tuzo ya mwaka huu amekua akikosolewa mara kwa mara kutokana na kuwa na hasira juu ya wachezaji wenzake.Wawrinka kamwe hawezi kutoa hotuba kama hiyo kwa adui yake mwenyewe.
No comments:
Post a Comment