Majenerali 2 waihama kambi ya Machar - LEKULE

Breaking

12 Aug 2015

Majenerali 2 waihama kambi ya Machar

Sudan Kusini
Majenerali wawili waasi nchini Sudan Kusini wametangaza kwamba wamejitenga na kundi la waasi linaloongozwa na Riek Machar.
Gathoth Gatkuoth na Peter Gadet wamesema kuwa sasa wanakabiliana na waasi hao pamoja na serikali mjini Juba.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini vilizuka mwaka 2013 kati ya vikosi vilivyo vitiifu kwa rais Salva Kiir na wapiganaji wa Machar aliyekuwa naibu wake.
Gathoth
Wapatanishi wa eneo hili wameweka makataa ya tarehe 17 mwezi Agosti kwa makubaliano ya amani kuafikiwa.
Haijulikani waasi hao wana wanajeshi wangapi,lakini wachanganuzi wanasema kuwa majenerali wote wawili wamekuwa na uwezo mkubwa ardhini na kujiondoa kwao kunaweza kuathiri pakubwa mazungumzo ya amani.

No comments: