Mabasi yaendayo haraka kuanza kujaribiwa leo Agosti 17 jijini Dar kwa vituo 10 - LEKULE

Breaking

17 Aug 2015

Mabasi yaendayo haraka kuanza kujaribiwa leo Agosti 17 jijini Dar kwa vituo 10

maba
Mabasi mawili yaliyoletwa nchini kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kama yanavyoonekana ambapo leo yanatarajia kuanza kwa safari ya majaribio katika baadhi ya vituo ikianzia Kimara mwisho hadi Posta. Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanatarajia kuonja usafiri huo ambao ni majaribio huku wahusika wakieleza kuwa watakuwa na muda muafaka wa kutoa elimu kwa watumiaji wa usafiri huo mpaka hapo watakapouzoea.

(Dar es Salaam). Asubuhi ya leo mabasi yaendayo haraka yanatarajia kuanza rasmi zoezi la majaribio ya usafirishaji wake wa abiria  safari inayotarajia kuanzia Ubungo jijini Dar.  Imeelezwa kuwa zoezi hilo litakuwa ni la muda kwa kipindi cha majaribio huku wahusika wakiwa na lengo la kutoa elimu kwa watumiaji wa usafiri huo na wata wapata fursa ya kuyapanda na kushuhudia namna ya ufanyaji wa kazi zake ambapo ruti zitatoka  Ubungo kwenda Kimara na kutoka Kimara hadi Kivukoni Bure.
Kwa mujibu wa DeusiDedith Mutasingwa afisa wa masuala ya fidia katika mradi wa mabasi hayo, anasema  mabasi ambayo kwa sasa yapo mawili, yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo yenye uwezo wa kubeba watu 80 huku yakitarajia kutumia dakika chache kufikia kila kituo na muda wa kupakia kisha kuondoka.
Aidha, anaendelea kueleza kuwa, mabasi hayo yametengenezwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo kwa wahusika ikiwemo watu wenye mahitaji maalum  wakiwemo Walemavu, Wajawazito. Hata hivyo alitoa onyo kali kwa wafanyabiashara waliopanga vitu vyao ndani na pembezoni mwa barabara hizo kuziondoa mara moja kwani watakaokiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo faini ya kuanzia sh.250,000.
Mradi huo wa mabasi yaendayo haraka  upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)  ambapo kwa hatua hiyo Tanzania kupitia jiji lake la Dar es salaam litakua miongoni wa majiji ya mwanzoni kutekeleza mradi huo mkubwa na kuwa ya kwaza kwa Afrika Mashariki.

No comments: