Jaji Mkuu wa Shindano la Tanzania
Movie Talents (TMT) Roy Sarungi akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mapema leo Katika ofisi za Proin Promotions Ltd juu ya
mchakato mzima wa fainali ya TMT itakayofanyika tarehe 22 August 2015
Katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa kiingilio cha Shilingi
Elfu Hamsini (50000) kwa viti maalumu na shilingi elfu thelathini
(30000) kwa viti vya Kawaida.Mshindi katika fainali hiyo itaondoka na
kitita cha Shilingi milioni hamsini (50,000,000) za Kitanzania.
Meneja Mradi wa Tanzania Movie
Talents (TMT) Saul Mpock akiongea kuhusu jinsi Fainali hiyo
itakavyorushwa ,moja kwa moja (live) kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii , Vilevile amewashukuru wadau
wote ambao wameweza kuipiga tafu TMT kwa mwaka huu na kuhaidi kuendelea
kukushirikiana nao kwa njia moja au nyingine.
Meneja Bidhaa wa Paisha Godfrey
Fataki ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents
(TMT) 2015 akiongelea juu ya wao kushawishika kuamua kuidhamini Paisha
mara baada ya kuona kuna umuhimu mkubwa wa kuinua sekta ya filamu nchini
huku akisisitiza Wananchi kutumia app ya paisha katika Simu zao
kwaajili ya kuweza Kujipatia bidhaa mbalimbali kutoka kwenye makampuni
mbalimbali ambayo yanapatikana ndani ya app hiyo ya Paisha.
Fainali ya Shindano la Tanzania
Movie Talents (TMT) 2015 itafanyika mnamo tarehe 22 August 2015 katika
ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kuanzia saa moja na nusu usiku huku
fainali hiyo ikirushwa live kupitia kituo cha ITV pamoja na mitandao
mbalimbali ya kijamii kama vile blogs.
Tiketi za fainali zinapatikana Makumbusho ya Taifa Posta, Kwenye Maduka yote ya Hussein Pamba Kali, Dar Live Mbagala, Shear Illusion Mlimani City na Millenium Tower na Tausi Fashion Mlimani City Shindano la TMT limedhaminiwa na Paisha huku wakisaidiwa na Pepsi, Camgas, Precision Air, ITV/Radio, Global Publishers, I-View Studio, Hartman Barbershop, Van Maria Boutique, Hussein Pamba kali, Data Vision International
No comments:
Post a Comment