Dk. Slaa apigwa 'STOP' CHADEMA..........Mbowe asema Wamempumzisha Kwa Muda Usiojulikana - LEKULE

Breaking

4 Aug 2015

Dk. Slaa apigwa 'STOP' CHADEMA..........Mbowe asema Wamempumzisha Kwa Muda Usiojulikana

Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe leo  amesema kwamba  chama cha Chadema kimempumzisha katibu mkuu wake Dk. Wilbroad  Slaa kwa muda  usiojulikana.

Akizungumza   katika mkutano wa baraza kuu Chadema Mbowe amesema kwamba chama cha Chadema kimekubaliana kumpumzisha Dr. slaa kwa muda lakini nafasi yake ya katibu mkuu katika chama hicho iko pale pale.

“Tumekubaliana kwamba katibu mkuu Dr. Slaa apumzike kwa muda na sisi  tuendelee atakapokuwa tayari ataungana na sisi mbele ya safari, chama hiki hakiendeshwi kwa siri tunakiendesha kwa mikakati” Amesema Mbowe

Ameongeza kuwa Chadema hakiwezi kuwa chama cha kuhubiri mabaya ya jana na kushindwa kuhubiri maendeleo ya kesho na kipigo wanachokipata CCM hawajawahi kukipata tangu nchi imeanza vyama vingi vya siasa.

Hivi karibuni kumekuwa na habari ambazo hazijathibitishwa zinazodai kwamba Dr.Slaa ni mmoja kati ya wanasiasa wasiokubaliana na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kuhamia katika chama  hicho suala linalopelekea kuto onekana katika vikao mbalimbali vya chama hicho vinavyo endelea jijini Dar es salaam.


Katika hatua nyingine Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa unatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais  ambaye  ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya chama  cha CHADEMA 

No comments: